Wanaharakati wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wameikosoa bajeti ya mwaka 2016/17 kutokana na kuzifanya Sh50 milioni zilizoahidiwa na Rais John Magufuli kwa kila kijiji, kuwa za mkopo badala ya kutolewa kama ruzuku.
Katika tamko lao, wanaharakati hao walisema Serikali itafute vyanzo vingine vya mapato ili iweze kutoa ruzuku kwa vikundi vya wanawake kwani walio wengi tayari wana mikopo wliyopewa na taasisi za fedha na hivyo wana mzigo wa madeni.
Akisoma tamko hilo, Janeth Mawinza alisema wanawake wana madeni mengi ambayo wameshindwa kulipa kwa sababu ya kukosa elimu ya kufanya biashara.
“Tuwape unafuu sasa kwa kuwapa ruzuku, vinginevyo tutawasababishia msongo wa mawazo kwa kudaiwa na taasisi mbalimbali za fedha,” alisema.
Alisema mpango huo wa mikopo bila kuwapa elimu ya biashara unaweza kusababisha vifo kwa baadhi yao.
“Tumeshuhudia wanawake wananyang’anywa samani zao na kusababisha msongo wa mawazo kwa sababu ya kukosa elimu ya biashara, tutawaua,”alisema.
No comments:
Post a Comment