Thursday, 24 August 2017

Dalala Lagonga Treni Morogoro Na Kuua Watu Kadhaa


SeeBait

Watu ambao idadi yake haijaweza kufahamika mara moja, wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa, baada ya daladala waliyokuwa wakisafiria kugonga treni mkoani Morogoro.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Urich Matei, amesema ajali hiyo imetokea leo asubuhi na imehusisha gari aina ya daladala yenye amba za usajili T 438 ADR iliyokuwa inakwenda Mvumi kwenye njia panda inayoingilia treni ndipo ikagonga treni hiyo, na kuburuzwa takribani mita 200.

Kamanda Matei amesema chanzo cha ajali hiyo ni daladala kuingia kwenye njia ya treni bila kusimama ili kuangalia kama kuna treni inakuja, ndipo treni hiyo ikaburuza gari hiyo kwa umbali mrefu na kusababisha maafa hayo.

Idadi rasmi ya majeruhi bado haijafahamika rasmi mpaka sasa na majeruhi wamepelekwa hospitali ya mkoa wa Morogoro


No comments: