Serikali
imewakaribisha wawekezaji kutoka nchini Cuba waje kuwekeza kwakuwa kuna
fursa nyingi hapa Tanzania na kama zitatumika vizuri basi zitawezesha
uchumi kuendelea kukua kwa kasi.
Hayo
yamesemwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mjini Havana nchini Cuba mara
baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Cuba, Lucas
Domingo Polledo, ambapo amewakaribisha wafanyabiashara wa Cuba kuja
kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya dawa.
Amesema
kwa sasa Serikali ya Tanzania inaagiza dawa kutoka nje ya nchi jambo
ambalo linasababisha kutumia fedha nyingi, hivyo uwepo wa kiwanda
utasaidia katika kupunguza gharama.
Majaliwa
ameongeza kuwa Serikali imedhamiria kuendeleza sekta ya viwanda nchini
kama mkakati wa kukuza uchumi na kufikia uchumi wa kati,
No comments:
Post a Comment