Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Nyakoro Sirro amefanya mabadiliko ya makamanda wa polisi mikoani.
Taarifa
ambayo imetolewa na msemaji wa Jeshi la Polisi Barnabas Mwakalukwa
imesema kwamba Sirro amemteua Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Juma Yusuf
Ally kuwa Kaimu Kamishna wa Polisi Zanzibar.
Uteuzi
huo unafuatia kustaafu kwa aliyekuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar
Kamishna Hamdani Omari Makame kwa mujibu wa sheria baada ya kutimiza
umri wa miaka sitini (60).
IGP
Sirro pia amemteua Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP)
Lazaro Mambosasa kuwa Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam.
Kabla ya uteuzi huo, SACP Mambosasa alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.
Kufuatia
uteuzi huo, aliyekuwa Kaimu Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam
anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, na aliyekuwa Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Mtwara Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP)
Neema Mwalimu Mwanga anakwenda Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam.
IGP
Sirro pia amemteua aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Gilles Bilabaye Mroto kuwa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)
Emmanuel Lukula kwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Temeke.
Kabla ya uteuzi huo, ACP Lukula alikuwa Ofisa Mnadhimu wa Polisi mkoa wa Mbeya.
Jeshi
la Polisi linatoa wito kwa wananchi wote kuendela kushirikiana na Jeshi
hilo kwa kufichua taarifa za uhalifu na wahalifu ili kwa pamoja
tuendelee kuiweka Tanzania salama.
No comments:
Post a Comment