Wakati
sakata la Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gelasius Byakanwa kumsweka mahabusu
mwalimu wa sekondari kwa kushindwa kutaja jina lake likiendelea kuzua
mjadala, imedaiwa kuwa siku hiyo aliwauliza walimu aliokuwa na kikao nao
maswali 22.
Tukio
hilo la Byakanwa kudaiwa kuamuru kukamatwa na kuwekwa mahabusu mwalimu
huo wa Shule ya Sekondari Lerai, Erasto Mhagama, ndilo limekuwa gumzo
katika mitandao ya kijamii.
Mbali
na kubamba mitandao ya kijamii, walimu katika mijumuiko mbalimbali na
kupitia Chama cha Walimu Tanzania (CWT) na makundi ya WhatsApp ya
walimu, tukio hilo ndilo linalojadiliwa zaidi katika mitandao hiyo.
Inadaiwa
baada ya mwalimu huyo kushindwa kuandika jina la mkuu wa wilaya,
kiongozi huyo alimtaka achague mojawapo ya adhabu kati ya kupiga pushup
20 au kwenda mahabusu ya polisi.
Mwalimu
huyo alimweleza mkuu huyo wa wilaya kuwa asingeweza kupiga pushup kwa
kuwa ana matatizo ya kiafya, ndipo mkuu wa wilaya alipoita polisi na
kumpeleka mahabusu.
Ilielezwa
kuwa katika kikao hicho na walimu wa shule mbili za sekondari Boma na
Lerai, mkuu huyo wa wilaya alianza kwa kugawa karatasi na kuwauliza
walimu kama kuna anayemfahamu.
Alipowauliza
swali hilo walimu wa Shule ya Lerai, ni mmoja tu aliyesema anamfahamu
ndipo alipowataka wengine wote kuandika jina lake kwenye karatasi.
Baadaye
alimsimamisha mwalimu mmoja baada ya mwingine akitaka waende ubaoni
kuandika maneno au kuweka majibu ya maswali atakayowauliza na maswali
hayo yalikuwa kama ifuatayo:
1.Nani ambaye ananifahamu?
2. Kila mmoja aaandike jina langu kwenye hiyo karatasi
3. Waziri mkuu wa awamu ya tatu ni nani?
4. Nitajie kirefu cha CDF (Chief of Defence Forces)
5. Nitajie Waziri wa Nishati na Madini
6. Andika kirefu cha DC (District Commissioner)
7. Andika neno IGP na kirefu chake
8. Andika neno CDF na kirefu chake
9. Andika CUF na kirefu chake
10. Andika CAF na kirefu chake
11. Andika neno Tanu na kirefu chake.
12. Andika TLP na kirefu chake
13. Agronomy means what?
14.
Nani ni viongozi wakuu wa CUF. Baada ya kujibiwa ni Profesa Ibrahim
Lipumba na Maalim Seif Sharifu Hamad akauliza mkutano wao mkuu wa mwisho
ulikuwa lini?
15. Nani ni kiongozi wa CAF (Confederation of African Football)
16. Nitajie IGP (Inspekta Jenerali wa Polisi) ni nani na CDF (mkuu wa majeshi) ni nani kwa majina
17. Mwenye cheo cha CDF ni nani
18. Mwamunyange mnamfahamu? Ni Nani
19. Baada ya kustaafu Mwamunyange akaja nani?
20. Mkuu wa Majeshi kwa Kiingereza anaitwaje?
21. Rais wa CAF ni nani?
22. Andika pale ubaoni Chief of Defence Forces
No comments:
Post a Comment