Mwalimu
wa shule ya msingi katika kata ya Ligunga tarafa ya Matemanga wilaya
Tunduru mkoani Ruvuma Rajabu Morisi amefikishwa katika Mahakama ya
wilaya hiyo kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wake na kumsababishia
ujauzito.
Akisoma
shauri hilo no 148/2017, mbele ya mlinzi wa amani hakimu wa Mahakama ya
mwanzo Itika Korosho, mwendesha mashtaka wa Mahakama ya wilaya Inspekta
Bosco Kilumbe amesema mtuhumiwa alitenda kosa hilo kati ya mwezi
January na Mei mwaka huu katika muda usiojulikana baada ya kumrubuni
mwanafunzi huyo.
Na
kudai kufanya hivyo ni kinyume cha sheria namba 130 (1) na (2e) na
namba 131 (1) na (2) vya sheria ya kanuni ya adhabu sura namba 16 kama
ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Hata
hivyo mtuhumiwa huyo amekana kosa hilo upelelezi bado unaendelea ,
mtuhumiwa yupo nje kwa dhamana, kesi hiyo itatajwa tena Mahakamani
Agosti 28 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment