Watu
32 wamefikishwa mahakamani kujibu shtaka la mauaji ya wanawake watano
yaliyotokea katika Kijiji cha Undomo Kata ya Uchama wilayani Nzega.
Miongoni
mwa waliofikishwa mahakamani jana Jumatatu na kusomewa shtaka mbele ya
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Nzega, Sarafina Nsana
wamo viongozi wa serikali ya kijiji hicho na wengine wa ngazi ya kata.
Mwendesha
Mashitaka wa Polisi, Melito Ukongoji aliiambia mahakama kuwa Julai 25,
washtakiwa kwa pamoja, wakiwa katika kijiji cha Undomo waliwashambulia
kwa kuwapiga na kuwachoma moto hadi kufa wanawake watano kwa tuhuma za
imani potofu za ushirikina.
Akisaidizana
na mwenzake, Agustino Nshimba mwendesha mashtaka huyo aliwataja
waliouawa katika tukio hilo kuwa ni Nsuku Masali, Ester Kaswahili,
Christina Saidi, Mwashi Mwinamila pamoja na Kabula Kagito.
Waliosomewa
mashtaka ambao hata hivyo hawakutakiwa kujibu lolote kwa sababu
mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza na kuamua mashauri ya
mauaji ni pamoja na Mtendaji wa Kata ya Uchama, Malewa Maroji, Diwani
wa Kata hiyo, Karoli Massanja, Kiongozi wa Sungusungu, Dotto
Saraganda, mwenyekiti wa kijiji, Ramadhani Kulwa na mtendaji wake,
Rauliani Sanyiwa.
Washtakiwa
wengine ni Dotto Saraganda (49), Taus Ngassa (40), Pill Kapewi (25),
Leons Sospeter (36), Issah Eliudi (20), Nhungulu Sospeter (25), Saidi
Nsabi(25), Emmanuel Pius(18), Estar Muhamila(25), Tatu Thomas (35),
Thotunatus Ngelera (30), Milika Daudi (36), Kisuge Ntemi(31), Kulwa
Kizinza (40), Shija Masali (35), na Kulwa shomali(31).
Wengine
ni Selelo Mashandete (46), Steven Saraganda (60), Paul Christoph (60),
Makuya Athumani(42), Peter Mapalala(21), Maganga Daudi (19), Omary
Seleli (20), Paul Emmanuel (51),Charles Kiberiti (26), Emmanuel Mihayo
(27), Shomali Nhyama (75), pamoja na Shija Shomali (20).
Shauri
hilo imeahirishwa hadi Septemba 4, itakapotajwa tena na muda wote
wakati washtakiwa wakisomewa mashtaka dhidi yao, jeshi la polisi
liliimarisha ulinzi kuzunguka eneo la mahakama.
No comments:
Post a Comment