Saturday, 26 August 2017

Tembo Avamia Kijiji......Aua Mtu Mmoja Kwa Kumkanyaga na Kujeruhi Mwingine


SeeBait
Kijana Emmanuel Ernest wa kitongoji cha Ilolo, Mvumi Misheni wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma, amefariki dunia baada ya kukanyagwa na tembo huku mwingine akijeruhiwa vibaya baada ya tembo huyo kuvamia mashamba ya zabibu.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema tembo huyo alikuwa akitafuta maji majira ya alfajiri hivyo baadhi ya wanakijiji baada ya kumuona walikusanyika na kupiga mayowe, kitendo kilichomfanya mnyama huyo kukasirika na kuanza kuwafukuza kabla ya kumkuta marehemu Emanuel akiwa na mdogo wake wakichimba mitaro ya mizabibu na kumkanyaga kifuani na kumvunja mbavu nne na kusababisha kifo chake.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mvumi Misheni, Peter Songoro, amethibitisha kupokea majeruhi wawili, akiwemo marehemu na mdogo wake Amani Joseph ambaye alikanyagwa mgongoni na kisha utumbo kutoka nje, kabla ya Emmanuel kufariki baadaye wakati akipatiwa matibabu.

No comments: