Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu leo August 25, 2017 imeutaka upande wa mashtaka
kukamilisha upelelezi wa kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili
Mfanyabiashara Yusuf Manji ili matokeo ya kesi hiyo yajulikane mapema.
Rai
hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya Wakili wa
Serikali, Wankyo Simon kueleza upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na
wataeleza hatua ulipofikia katika tarehe itakayopangwa tena.
Baada
ya kueleza hayo, Hakimu Simba aliutaka upande wa mashtaka kuhakikisha
wanajitahidi kukamilisha upelelezi ili matokeo yake yajulikane mapema
ambapo aliahirisha kesi hiyo hadi August 31, 2017.
Mbali
ya Manji washtakiwa wengine ni Deogratius Kisinda, Abdallah Sangey na
Thobias Fwere ambao wanakabiliwa na mashtaka saba chini ya sheria ya
Uhujumu Uchumi na Usalama wa Taifa kwa kukutwa na vitambaa
vinavyotengeneza sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania vyenye thamani ya
zaidi ya Tsh Milioni 200 na mihuri.
No comments:
Post a Comment