Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro linamshikilia dereva wa basi lenye
namba za usajili T 438 ADR Charles Diamond, kwa kusababisha ajali
iliyopoteza uhai wa watu mkoani Morogoro na kusababisha majeraha kwa
baadhi ya watu.
Akitoa taarifa ya ajali hiyo iliyotokea leo asubuhi Kamanda wa Polisi
mkoani humo Urlich Matei, amesema mpaka sasa idadi kamili ya watu
waliofariki kutokana na ajali hiyo ni watu watatu, ambapo wawili ni
wanawake na mmoja ni mwanaume, huku mmoja wao akiwa ni mwanafunzi.
Majeruhi wa ajali hiyo ni 27 ambao wamepelekwa hospitali ya mkoa wa
Morogoro, lakini suala la utambuzi wa miili ya marehemu bado
halijafanyika mpaka pale uchunguzi utakapofanyika.
Ajali hiyo imetokea leo asubuhi iliyohusisha gari aina ya daladala
ikielekea Mvumi kugonga treni iliyokuwa ikipita kwenye njia yake,
kulikopelekea kuburuzwa kwa gari hiyo na kusababisha vifo.
No comments:
Post a Comment