Jumuiya
ya Wanawake wa Chama cha Wananchi (JUKECUF) imesema kuwa kuna mkakati
wa chini kwa chini ndani ya upande wa Prof. Lipumba wa kuandaa mkutano
mkuu iliouita ni bandia kwa ajili ya kumvua uanchama, Katibu Mkuu wa
chama hicho, Maalim Seif Shariff Hamad.
Hayo
yalisemwa jana na Mwenyekiti wa JUKECUF, Fatma Ferej alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za chama hicho
zilizopo Vuga mjini Unguja.
Ferej
alisema kwamba mkutano huo unaoratibiwa na upande wa Lipumba ni batili
kwa sababu siyo kiongozi wa chama hicho na kwamba maazimio ya mkutano
huo pamoja na mkutano wenye vitakuwa ni batili kwani hawana mamlaka.
Akitaja
lengo kuu la kumvua uanachama Maalim Seif, Ferej alisema ni ili
kuiondoa CUF katika kusimamia madai yake ya ushindi wa uchaguzi mkuu wa
Oktoba 25, 2015 ambao matokeo yake yalifutwa baada ya CUF kuibuka
ushindi.
Aidha,
jumuiya hiyo imetoa tahadhari kwa vyombo vya dola pamoja na Ofisi ya
Msajili wwa Vyama vya Siasa kuheshimu maamuzi ya chama hicho kwani
wajumbe wa mkutano mkuu wanafahamika kama walivyopatikana kupitia
Uchaguzi Mkuu wa CUF wa mwaka 2014 na si vinginevyo.
Mkurugenzi
wa Uchaguzi na Oganaizesheni, Nassor Seif aliyeteuliwa na Prof. Lipumba
amejibu tuhuma hizo zilizotolewa na JUKECUF na kusema kwamba tuhuma
hizo ni za uongo mtupu na kuwataka wananchi kuzipuuza.
No comments:
Post a Comment