Mwanaume
mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kumteka mtoto wakike
aitwaye Khailati Bashiri (8) ambaye ni mwanafunzi wa darasa pili katika
Shule ya msingi ya Iloganzala mkoani Mwanza.
Kamanda
wa Polisi mkoani Mwanza, DCP Ahmed Msangi amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa
ni Emmanuel Kirumbas (25) mkazi wa Malampaka mkoani Shinyanga ambapo
majira ya 6:00 mchana ya tarehe 21.08.2017 alimchukua mwanafunzi huyo na
kumpeleka kusikojulikana na baadae kutuma taarifa kwa njia ya simu
kwamba apatiwe fedha kiasi cha Milioni 3 ili aweze kumrudisha mtoto
huyo.
Inasemekana
kuwa baada ya mtoto huyo kutoka shuleni alikwenda nyumbani kwao mtaa wa
Iloganzala anapoishi na wazazi wake kubadilisha nguo kisha aliondoka na
kuelekea kusikojulikana, na kusababisha wazazi wake kuhangaika
kumtafuta bila ya mafanikio ndipo walipoamua kutoa taarifa kituo cha
Polisi.
DCP
Msangi amesema baada ya kupokea taarifa hizo jeshi la polisi lilifanya
upelelezi ambao ulipelekea kuwakamata watu watano na baadae kufanikiwa
kumkamata mtekaji nyara ambae alikuwa akihitaji kulipwa fedha.
Jeshi
la Polisi lipo katika mahojiano na mtuhumiwa na pindi uchunguzi
utakapokamilika mtuhumiwa aliyehusika na utekaji atafikishwa Mahakamani.
No comments:
Post a Comment