Jeshi
la Polisi mkoani Tabora linawashikilia wanafunzi 106 wa shule ya
Sekondari ya Milambo kwa madai ya kufanya vurugu na kujeruhi wananchi
zaidi ya sita katika eneo la jirani na shule hiyo.
Wanafunzi
hao wa kidato cha sita wamefanya vurugu hizo usiku baada ya kutoroka
shuleni na kuvamia kwenye sherehe ya harusi ambapo walitaka sherehe hiyo
iendelee hadi muda watakao amua wao.
Akizungumzia
tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani humo, SACP Wilbroad Mutafungwa
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo ameeleza kuwa wanafunzi hao
106 wanashikiliwa na jeshi la polisi kuhusiana na tukio hilo.
No comments:
Post a Comment