Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania Bara, Thobias
Andengenye amefanya mabadiliko ya baadhi ya Makamanda wa Mikoa na Wakuu
wa Vitengo wa Jeshi hilo.
Katika
mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa
Arusha Kamishna Msaidizi (ACF), Bakari Mrisho amekuwa Mkuu wa Chuo na
Mafunzo, nafasi yake inachukuliwa na Mrakibu (SF) Kennedy Komba, ambaye
alikuwa Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Iringa na nafasi yake inachukiliwa
na Mrakibu Msaidizi (ASF), James John toka Makao Makuu.
Kamanda
wa Mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi (ACF), Gilbert Mvungi, amekuwa
Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Kigoma, nafasi yake inachukuliwa na
Kamishna Msaidizi (ACF), Baraza Mvano ambaye alikuwa Kamanda wa Zimamoto
Mkoa wa Kigoma.
Kamanda
wa Viwanja vya Ndege Nchini, Kamishna Msaidizi (ACF), Juma Kwiyamba
amehamishiwa Makao Makuu, nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi
(ACF) Christom Manyologa.
Kamishna
Msaidizi (ACF) Fikiri Salla amekuwa Kamanda wa Mkoa wa Mbeya, anajaza
nafasi iliyokuwa wazi baada ya Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Mbeya
kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu
wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Kamishna
wa Usalama dhidi ya Moto.
Kamanda
wa Zimamoto Mkoa wa Pwani, Mratibu Msaidizi (ASF) Goodluck Zelote
amekuwa Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Tanga, nafasi yake inachukuliwa na
Mrakibu Msaidizi (ASF) Happy Shirima toka Makao Makuu.
Mratibu
Msaidizi (ASF), Fatma Ngenya amekuwa Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa
Manyara, anachukua nafasi ya Mkaguzi Msaidizi (A/INSP) Heriel Kimaro
ambaye amehamishiwa Makao Makuu.
Uhamisho
huo ni Mabadiliko ya kawaida yanayotokea ndani ya Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji, katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.
No comments:
Post a Comment