Akizungumza na wanahabari katika makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar es
salaam leo, kuhusu miaka 53 tangu kuasisiwa kwake, Mkuu wa Majeshi
Nchini, Jenerali Venance Mabeyo, amesema, wakati JWTZ inaandika historia
ndefu imefikia mafanikio mbalimbali, ikiwemo kudumisha amani na utulivu
uliopo nchini tangu Uhuru, limeshiriki Vita vya ukombozi Kusini mwa
Afrika, Vita vya Kagera na Visiwa vya Comoros.
Jenerali Mabeyo amesema, JWTZ pia limekuwa ni nguzo muhimu katika
kudumisha amani sehemu mbalimbali duniani kwa kushiriki katika shughuli
za Ulinzi wa Amani, katika nchi za Liberia, DRC, Sudan , Lebanon, Sudan
Kusini, na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Aidha, amemshukuru Rais Dk. John Pombe Magufuli, Baraza la
Mawaziri,pamoja na Viongozi Wakuu wa Serikali kwa Maelekezo mbalimbali
wanayoyatoa kwa Jeshi ushauri ambao umekuwa muhimili mkubwa kwa utendaji
wake.
No comments:
Post a Comment