Benki
ya Dunia (WB) imeipatia Tanzania mkopo wa Dola za Marekani 150 milioni
sawa na Sh336 bilioni kwa ajili ya kusaidia uhifadhi wa mazingira na
kukuza utalii wa asili katika maeneo ya mikoa ya kusini mwa nchi.
Fedha
hiyo ilitolewa na Shirika la maendeleo la kimataifa la benki hiyo (IDA)
kupitia mradi wa uhifadhi wa mazingira kwa ajili ya utalii (REGROW)
baada ya kuidhinishwa wiki iliyopita.
Fungu
hilo litakalotumika kwa miaka sita, kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo
vya habari iliyotolewa jana, litazinufaisha kiuchumi kaya takriban
40,000 zilizopo katika hifadhi kwa kuwa kutajengwa miundombinu na fursa
mpya za kiuchumi kwa lengo la kuongeza usimamizi wa hifadhi za asili.
Mpango
huo una lenga kukuza uhifadhi wa mapori ya Taifa, mbuga, maporomoko ya
mto Ruaha na kupunguza mwingiliano wa kimakazi kati ya binadamu na
wanyama pori.
Maeneo
yatakayohusika na mpango huo ni Mbuga za Katavi, Kitulo, Mahale, milima
ya Udzungwa, Mikumi na Ruaha, Pori la Selous, Mito inayopitiwa na bonde
la ufa (Nyansa na Tanganyika) .
Kuhusu
Mpango huo, Mkurugenzi wa Benki ya Dunia wa nchi za Tanzania, Malawi,
Somalia na Burundi, Bella Bird alisema utalii ni eneo muhimu kwa
maendeleo ambalo linaweza kuongeza ukuaji wa uchumi wa Tanzania kwa
asilimia 10 ya pato la Taifa (GDP) kwa hesabu za mwaka 2015.
“Nchi
hii imejaliwa wanyama wengi na vivutio vya asili lakini
vinavyotambuliwa na kujulikana zaidi ni vile vya maeneo ya Kaskazini mwa
nchi. Kuanza kuyajali maeneo haya ya kusini kutaongeza idadi ya
watalii, hivyo kuongeza faida za kiuchumi,” alisema Bird.
Alisema
Tanzania imefanikiwa kuongeza idadi kubwa ya watalii ndani ya muda
mfupi kutoka watalii 500,000 kwa mwaka 2000 hadi watalii zaidi ya
milioni moja kutokana na kuvitangaza vivutio vyake.
“Ukaichilia
mbali sifa ya kutunza vivutio, Serikali inapata mapato na sekta hii
hutoa ajira nyingi, mpaka sasa Tanzania ni zaidi ya watu 400,000
walioajiriwa katika sekta hiyo,” alisema Bird.
Kwa
upande wake mtaalamu wa mazingira wa Regrow, Daniel Mira alisema endapo
eneo hilo la kusini litafanywa kuwa maalumu kwa vivutio Tanzania
itakuwa imejiimarisha katika utalii.
“Hata
mapato yatakayokuwa yakipatikana yatakuwa na uwezo wa kuendeleza
vivutio vya kipekee jambo ambalo litalifanya eneo hilo kuwa kitovu cha
ukuaji wa kikanda na la mfano,” alisema Mira.

No comments:
Post a Comment