Upande
wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi, inayomkabili Mkurugenzi wa
Tathmini, Archard Alphonce Kalugendo (49) na Mthamini wa Madini ya Almas
wa Serikali, Edward Joseph Rweyemamu (50) umeileza mahakama kuwa,
sehemu kubwa ya upelelezi umekamilika bado maeneo machache.
Wakili
wa Serikali, Wankyo Simon alimeeleza hayo leo mbele ya Hakimu Hakimu
Mwandamizi, Godfrey Mwambapa wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kesi
hiyo ilipofika kwa ajili ya kutajwa.
Wakili
Wankyo amedai wanakamilisha upelelezi katika sehemu ndogo iliyobakia
na wamewaelekeza polisi kufanya hill na kwamba tarehe ijayo wataieleza
mahakama hatua ya upelelezi ilipofikia
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 26, itakapokuja kwa ajili ya kutajwa
Washtakiwa
hao wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa kusababisha hasara ya
dola za Kimarekani 1,118,291.43 sawa na Sh 2,486,397,982.54.
Kalugendo ambaye ni Mkazi wa Kinyerezi na Rweyemamu Mkazi wa Mwananyamala wote ni waajiriwa wa Wizara ya Nishati na Madini.
No comments:
Post a Comment