Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Ndg. Geoffrey Mwambe amesema
kwamba taarifa zilizotolewa na Mwandishi wa FT. John Aglionby kuhusu
mazingira ya Uwekezaji Tanzania kuwa yanatishia wawekezaji si sahihi na
yanalenga kupotosha ukweli kuhusu hali halisi kuhusu Uwekezaji Tanzania.
Mwandishi
huyo wa Financial Times ametoa maelezo ambayo amesema yametolewa na
Muwekezaji Aliko Dangote maelezo ambayo yamelenga kusukuma Agenda yake
ambayo haijulikani na yenye lengo la kupotosha sera za uwekezaji na
kuwaogopesha wawekezaji ambao wameendelea kuiamini Tanzania na kuwekeza
mitaji yao mikubwa hapa nchini.
Hatuamini
kuwa Ndugu Dangote anaweza kuwa msemaji wa kuhusiana na sekta ya madini
kwa hapa nchini. Amewekeza kwenye sekta ya viwanda na serikali imekuwa
mstari wa mbele kusikiliza na kuyafanyia kazi maoni ya mfanyabiashara
huyo ili kuweza kuboresha mazingira yetu ya uwekezaji hapa nchini.
Serikali yetu imejidhatiti katika kuboresha mazingira ya uwekezaji na
imedhamiria kuhakisha uwekezaji huo unakuwa na faida kwa watanzania nan
chi kwa ujumla.
Tunaamini
kuwa kuna umuhimu wa kuhakikisha maelezo yanakuwa na pande mbili ili
kuondoa utata utaojitokeza wa maelezo ambayo yanaweza kuathiri na
kusababisha utata kwa wafanyabiashara walioiamini Tanzania kama sehemu
yao ya kufanya uwekezaji. Tanzania inathamini na kujali wawekezaji wa
aina ya ya Aliko Dangote na mara nyingi tumekuwa tukiwasikiliza na
kufanyia kazi maoni yao ili kurekebisha sera ili ziweze kuwa na manufaa
kwa wote yaani waTanzania na wawekezaji. Kuna sera pamoja na sheria
ambazo tumezifanyia marekebisho ili ziweze kuwa na manufaa kwa wote.
Hivi
karibuni ni vizuri kufahamu kwamba DIL ilikuwa na matatizo mbalimbali
na serikali iliweza kukaa na Dangote na kusikiliza matatizo yao na
kutatua changamoto kadhaa zilizokuwa zinakwamisha uzalishaji katika
kiwanda chake cha Saruji na kufikia muafaka wa kutatua matatizo yote
ambayo kiwanda ilikuwa ina TIC pia imeanzisha juhudi maalum za kuhakisha
kuwa huduma zinotolewa kwa wawekezaji zinaboreshwa ili kuweza
kurahisisha utoaji wa huduma kwa ufanisi na kwa haraka. Kituo kimeweza
kuanzisha Kamati Maalum ya Kitaifa ya Kuhudumia wawekezaji yaani NIFC
ambapo matokeo makubwa yameweza kuonekana kutokana na uboreshwaji wa
huduma zetu chini ya mahali pamoja .
Tunamshukuru
sana Mh. Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta John Pombe
Magufuli kwa juhudi zake za dhati za kupambana na rushwa juhudi ambazo
zimeweza kuleta mafanikio n ahata kuifanya Tanzania kutajwa na ripoti
mbalimbali za dunia kama mahala bora Zaidi pa kuwekeza Afrika. Zaidi ya
ripoti tano zimeweza kuitaja Tanzania kwa mwaka huu pekee kama sehemu
bora Zaidi ya mazingira ya uwekezaji Afrika. Tunajivunia juhudi kubwa
sana alizozionyesha Rais wetu Mh.John Pombe Magufuli katika kuvutia
uwekezaji nchini hasahasa katika kutokomeza rushwa, jambo ambalo
mwandishi wa makala hiyo kwa sababu zake binafsi ameshindwa kuziweka
bayana.
Ni
muhimu sana kuelewa kuwa suala la kuwa na sera nzuri za uwekezaji kwa
manufaa ya mwekezaji na nchi limepewa kipaumbele kikubwa na Serikali ya
Awamu ya Tano. Tunahitaji sekta binafsi kutekeleza majukumu yake kwa
kufuata sheria na taratibu, mfano kulipa kodi stahiki wakati Serikali
kwa upande wake ikiendelea kuboresha zaidi mazingira ya biashara na
uwekezaji nchini. Katika makala yaliyotolewa na FT imejionyesha waziwazi
kuwa mwandishi hafahamu vizuri Sheri ya Uwekezaji ya Mwaka 1997.
Sheria
za Tanzania zinatambua umiliki binafsi wa mali na kuzuia uwezekano wa
kutaifisha mali hizo bila sababu za msingi za kisheria. Vilevile
Tanzania ni mjumbe wa Multilateral Investment Guarantee Agency (MIGA)
ambapo makubaliano ya wajumbe ni kutoruhusu utaifishwaji wa mali za
uwekezaji pamoja na Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro ya
Kibiashara (ICSID).
Tanzania
inaendelea kuhamasisha uwekezaji nchini na Kituo cha Uwekezaji kimekuwa
mstari wa mbele katika kushawishi wawekezaji na mashirika makubwa ya
kimataifa ambayo tayari yana uwekezaji nchini kuongeza mitaji yao.
Tanzania imeendelea kupokea wawekezaji wengi ambapo uwekezaji huo
umesaidia katika kukuza uchumi katika Nyanja mabilimbali mfano kuzalisha
ajira mpya na kuongeza mapato ya kikodi. Matokeo haya chanya yanatokana
na juhudi za Serikali kujenga mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji
nchini.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TIC amewashukuru wawekezaji waliowekeza mitaji yao Tanzania
kwa ushirikiano wao mzuri na kuwaahidi kuwa Serikali itaendelea na
juhudi zake za kuboresha mazingira ya uwekezaji ikiwa ni pamoja na
kuboresha mfumo mzima wa kuwahudumia wawekezaji.
Ili
kuhakikisha kuwa nchi yetu inaendela kuwa na mazingira mazuri ya
uwekezaji, Serikali imeipa kipaumbele utekelezaji wa miradi ya
miundombinu wezeshi ili kusaidia katika kupunguza gharama za uwekezaji.
Baadhi ya miradi hii ni pamoja na Mradi wa kuzalisha umeme wa Stiegler’s
Gorge, ujenzi wa barabara, ukarabati wa miundombinu ya Bandari ya Dar
es Salaam (Gati 1-7), ujenzi wa Reli ya Kati kwa iwango cha standard
gauge. Jitihada nyingine zilizofanyika hivi karibuni ni uanzishwaji wa
Mfuko wa Benki ya Ardhi (Land Bank Fund) na kuboresha mfumo wa asajili
wa makampuni BRELA.
Tanzania
imeendelea kufanya vizuri kwenye kuvutia uwekezaji ukilinganisha na
nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki. “Tanzania imo katika
orodha ya nchi kumi bora Afrika zinazovutia uwekezaji kulingana na
ripoti ya Rand Merchant Bank (RMB). Vilevile Tanzania imeendelea kuwa na
kiasi kikubwa cha mitaji ya uwekezaji kutoka nje ya nchi (foreign
direct investment) ukilinganisha na nchi nyingine za Jumuiya ya Africa
Mashariki” amesema Bw.Mwambe
No comments:
Post a Comment