Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Mkazi
wa Mtaa wa Mbete,Kata ya Isanga Jijini Mbeya Bwana Yussuf
Hamad(39),anatuhumiwa kumpa mimba binti yake wa kumzaa(15) jina lake
limehifadhiwa.
Hayo
yamethibitishwa na Mama mzazi wa binti huyo Bi, Regina Simon(35) baada
ya kupata taarifa Mei 11 mwaka huu kuwa binti yake ana ujauzito wa miezi
minne,na kuamua kutoa taarifa kwa Balozi wa mtaa huo Bwana Steven
Ovaova ambaye naye alitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kitongoji Bwana
Angelo Sanga.
Viongozi
hao wa mtaa walimuita mtuhumiwa na ili kupata ukweli wa tukio
hilo,lakini mtuhumiwa alikanusha ingawa binti yake alithibitisha
kutendewa ukatili huo na kwamba alikuwa akitishiwa kwa mapanga kila
alipokuwa akifanya naye tendo la ndoa.
Baada
ya uongozi kupata maelezo kutoka kwa binti huyo na mzazi kukataa
waliamua kuipeleka kesi hiyo Polisi,ambapo walitoa PF3 iliyomwezesha
binti huyo kupelekwa kwa daktari ambaye alithibitisha kuwa binti huyo
ana ujauzito.
Hata
hivyo hivi sasa binti huyo amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya
akisubiri kujifungua ingawa umri mdogo wa binti huyo amekuwa chini ya
uangalizi wa karibu wa daktari hospitalini hapo.
Mtuhumiwa
atafikishwa mahakamani Septemba 25 mwaka huu katika mahakama kuu jijini
hapa,ili kujibu tuhuma zinazomkabili kesi inayotarajiwa kusikilizwa na
hakimu wa mahakama hiyo mheshimiwa Majige.
No comments:
Post a Comment