CHADEMA Yazidi Kuitafuna Familia Ya Wasira
Baada
ya kamanda Makongoro Wasira kujiunga na M4C siku chache zilizopita, leo
tena watoto wengine wa Wasira wamejiunga na M4C na kukitupia virago
Chama cha Baba yao CCM. Waliojiunga leo katika Makao makuu ya Chadema na
kukabidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa Chadema Dr Slaa ni kamanda Ester
Wasira na Lilian Wasira.
Wakizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa kadi walikuwa
na haya ya kusema:Ester wasira: (Ni mwanasheria, graduate wa UDSM)
(i) Chadema ni Chama cha kizalendo na mkombozi wa dhati wa Mtanzania.
(ii) Chadema kinaleta matumaini mapya kwa Watanzania hasa vijana wasio
na kazi na matumaini, Watanzania wenye maisha magumu hata kushindwa
kumudu milo miwili kwa siku, akina mama wanaohangaika vijijini bila
matibabu ya uhakika, maji, umeme, nyumba bora nk
(iii) CCM imedumaza nchi, nchi imekuwa kama mtu aliyedumaa kwa kukosa
protein, haikui tena, Chadema ni damu mpya yenye kuweza kuingiza protein
kwenye mishipa ya nchi iweze kufufuka na kukua tena.
(iv) Chadema kina viongozi imara na kwa maneno na matendo yake
wanawadhihirishia watanzania kuwa ni waadilifu na wana nia njema ya
kuipeleka Tanzania mbele. Alimalizia kwa kuwaasa vijana, akina mama na
wazee wajiunge na M4C ili kuijenga Tanzania mpya. Alimalizia kwa kusema,
“Kwa msaada wa Mungu, Tanzania Mpya inakuja.
Lilian Wasira (Mwanasheria, graduate wa TUDARCO):
(i) Alielezea furaha yake kwa kujiunga na Chama makini na chenye kuleta
matumaini mapya kwa mtanzania
(ii) Aliwaasa vijana, akina mama na wazee wajiandikishe kwa wingi nafasi
itakapotokea na 2015 wakamalizie kazi ya ukombozi kwa kuipigia Chadema
kura
(iii) Amewaasa Watanzania kuacha kulalamikia maovu ya CCM na kuchukua
hatua ya kuiweka CCM pembeni na kuleta Chadema kama chama mbadala.
Alisema hakuna sababu ya kuwa na mfumo wa vyama vingi kama watanzania
hawathubutu kuchagua chama mbadala na badala yake kuendelea kuichagua
CCM na kulalamika kila siku kuwa CCM imeshindwa kuongoza nchi
(iv) Kwamba CCM imekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 50 hivyo ni wakati
sasa wa kuiweka pembeni na kuingiza chama kipya, mawazo mapya na
kujenga mfumo mpya wa uongozi. Hakuna kitu CCM imeshindwa kufanya kwa
miaka 50 inaweza kufanya kwa miaka 5 au 10 ijayo.
(v) Anasema ana imani na sera za chadema kuwa ndizo zitatukomboa.
Amewapa moyo viongozi wa Chadema wasitishwe na vitisho na mauaji
yanayofanywa na dola na kusema yupo tayari kwa M4C na yupo tayari
kulipuliwa kama walivyolipuliwa wanachadema wengine na kuuawa kama
itambidi afanye hivyo.
(vi) Kwamba Chadema ni Chama kinachosubiri kuingia Ikulu isipokuwa tu
watu wajiandikishe, wapige kura na walinde kura.
(vii) Nae alimalizia kwa kusema “Kwa msaada wa Mungu Tanzania mpya
inakuja.”Dr Slaa alitiwa moyo sana na ujasiri ulioonyeshwa na vijana
hawa pamoja na maneno ya kizalendo waliyoongea na akawakarisha kwenye
uwanja wa mapambano ya M4C.
No comments:
Post a Comment