Na. Issa Mtuwa
STAMICO
Wananchi wameiomba serikali kuhakikisha rasilimali za Madini
zinawanufahisha Watanzania wote na sio wachache wenye uwezo. Kauli
ambayo imewahi kutolewa siku za hivi karibuni na Waziri wa Nishati na
Madini Prof. Sospeter Muhongo.(MC)
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti wakati walipotembelea katika banda la Shirika la
Madini la Taifa STAMICO katika maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa
(SABASABA) 2014, wananchi hao wamesema ili azma hiyo iweze kutimia ni
vyema Serikali ikaijenga uwezo STAMICO kifedha na vitendea kazi ili
iweze kutekeleza miradi ya uchorongaji na uchimbaji madini
itakayowanufaisha wananchi.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake alioambatana nao katika banda la
STAMICO, Mkazi wa mkoa wa Mara, Bw. Joel M. Changarawe amesema katika
kujenga uwezo wa kifedha wa Shirika hilo, Serikali haina budi kuendeleza
azma yake ya kuikabidhi STAMICO migodi yote mikubwa ya Madini iweze
kumiliki kwa niaba ya Watanzania na kuzalisha ili kuongeza tija kwa
Taifa.
Jacqueline
Aisaa akitoa maoni yake kuhusu sekta ya Madini wakati wa maonesho ya 38
ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba 2014. Anae msikiliza ni Bw. Issa
Mtuwa Afisa Uhusiano wa STAMICO. “Nashauri Watanzania tuache ubinafsi na
ubepari.
Naishauri serikali Migodi yote ya Madini yenye RESERVE (akiba) kubwa
imilikiwe na STAMICO kwa niaba ya Watanzania badala ya kukabidhi kwa
Watanzania wachache wenye tamaa ya utajiri ambao wanamiliki vitalu vya
madini kupitia migongo ya kampuni za kigeni” alisema Bwana Joel kwa
kuandika kwenye kitabu maalum cha Maoni, ushauri na kero za Wananchi.
Naye
Jacqueline Aisaa mkazi wa Masama-Moshi, ambaye pia ni mwanafunzi wa
mwaka wa tatu wa Shahada ya kwanza katika Chuo cha usimamizi wa fedha
(IFM) alisema serikali iipe meno STAMICO ya usimamizi wa hisa zote za
serikali kwenye migodi yote na usimamizi wa jumla katika sekta ya Madini
ili Wananchi waweze kunufaika na raslimali hizo.
No comments:
Post a Comment