Wednesday, 24 June 2015

Urais 2015: Membe Awataka Wenzake Kuheshimu Matokeo


WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amewataka wenzake wanaowania kuteuliwa na CCM kugombea urais wa Tanzania kuwa tayari kuyaheshimu matokeo yatakayoamuliwa na Kamati Kuu, Halmashauri Kuu ya Taifa na Mkutano Mkuu wa CCM katika mchakato wa kumpata mgombea bora wa chama hicho baadaye mwezi ujao.
 
Kutokana na maamuzi ya vikao hivyo amesema asitokee mtu wa kuwahusisha na mtu au kikundi chochote kutoka miongoni mwao kwa kuwa maamuzi ya wajumbe wa mikutano hiyo ni ya mwisho, hivyo lazima kila mmoja ayatii.
 
Membe aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wananchi na wanaCCM waliofurika Ofisi ya CCM Wilaya ya Morogoro Mjini Kichama kwa ajili ya kudhaminiwa fomu zake za kuomba kuteuliwa mgombea wa Urais Oktoba mwaka huu.

No comments: