Wakizungumza katika ibada ya maadhimisho ya miaka 50 ya kanisa la
Anglikan mkoani Morogoro waumini hao wamesema watanzania wanatakiwa
kuchagua viongozi wenye hofu ya mungu na watakao idumisha amani ya
Tanzania alio tuachia Bwana wetu Yesu Kristo ambapo wamewataka wakristo
kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi serikalini katika
chaguzi zijazo.
Kwa upande wao viongozi wa kanisa la Anglikani wa Dayosisi ya
Morogoro Askofu Godfrey Sehaba amewataka wakristo kuwachagua viongozi
wenye hofu ya mungu huku kaasisi wa kanisa la Anglikan Berega Aizack
mgego amesema kuwepo kwa watangazania walio na elimu ya chini kuna
sababishwa na viongozi wengi ambao wana elimu za juu kushindwa kuiongoza
nchi katika haki na kuwapigania wanyonge.
No comments:
Post a Comment