Mwenyekiti
wa (CHADEMA) na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe amefunguka na kusema ni
upambavu mkubwa kutumia zaidi ya milioni mia saba kwa ajili ya kufanya
marudio ya uchaguzi wa udiwani wa kata tatu baada ya madiwani wa CHADEMA
kudaiwa kununuliwa na CCM.
Mbowe
amesema hayo juzi alipokuwa akiongea na wakazi wa Machame Uroki akiwa
kwenye ziara yake jimboni Hai na kusema fedha ambazo zinakwenda kwa
ajili ya uchaguzi wa marudio zingeweza kufanya mambo mengine ya msingi.
"Gharama
ya kurudia uchaguzi wa diwani mmoja ni shilingi milioni mia mbili
hamsini, madiwani watatu waliopewa fedha wakaikimbia CHADEMA wakawaacha
wananchi huo ni usaliti gharama ya kurudia uchaguzi kwenye kata tatu ni
milioni mia saba na hamsini.
"Hizi
ni pesa zenu, hizi ni pesa za Watanzania pesa hizi zingetumia kujenga
shule ya msingi kwa Kasagile, hizi ni pesa zingetumika kujenga barabara,
tunaacha kujenga hospitali tunakwenda kuzitumia fedha hizi kwenye
uchaguzi milioni mia saba na hamsini ni upumbavu mkubwa" alisema Mbowe
Hata
hivyo Mbowe amesema kuwa licha ya madiwani hao kununuliwa hata uchaguzi
ukifanyika kesho anaamini kuwa chama chake kitaibuka na ushindi kwa
kata zote tatu
"Niwaambie
tu CCM haki ya Mungu hizo Kata tatu haiondoki hata moja labda watu wa
Uroki mniambie mko tayari tuwaachie hizo Kata, tutakesha usiku tutakesha
mchana haipotei Kata hata moja waite uchaguzi hata kesho, kuna watu
wanafika bei tuachane nao tuna mambo ya kupigana katika maisha yetu" alisisitiza Mbowe
Madiwani
wa tatu wa jimbo la Hai walijiuzulu nafasi zao na kusema wanamuunga
mkono Rais Magufuli na serikali ya awamu ya tano kutokana na utendaji
wake madiwani hao ni pamoja na Diwani wa Kata ya Machame Magharibi,
Goodluck Kimaro, Diwani wa Kata ya Weruweru, na Diwani wa Kata ya
Mnadani, Everist Peter Kimati ambao wote wamejiunga na CCM.
No comments:
Post a Comment