KAMANDA
wa polisi mkoani Pwani,(ACP) Jonathan Shanna (Pichani Kulia), amesema
kuanzia sasa watataifisha mali zote za watu wanaojihusisha na biashara
ya usafirishaji wa wahamiaji haramu.
Aidha amewatahadhalisha wale wanaotoa vyombo vyao vya majini na nchi kavu kusafirisha wahamiaji hao kwani navyo vitataifishwa .
Akizungumzia
hatua walizozichukua kwa wahamiaji haramu 72 waliokamatwa mapema wiki
hii,kamanda Shanna alisema kushiriki kwenye biashara hiyo ni kosa la
kubwa la kijinai.
Amesema
wanaojihusisha kusaidia na kuwawezesha kufika wahamiaji haramu
watawachunguza mali mbalimbali walionazo kama imetokana na utakatishaji
fedha na endapo itabainika imetokana na biashara hiyo zitafilisiwa.
Kamanda
Shanna alibainisha,wataiomba mahakama kutaifisha mali zote za wale
watakaobainika kuhusika kupata mali hizo na fedha na biashara haramu.
Amesema
sheria ipo wazi inasema watu hao wapewe kifungo ama kupigwa faini hivyo
itapendeza na itafurahisha jeshi la polisi kama watakuwa wanapewa
adhabu zote na kufungwa .
Kamanda
Shanna ,alisema taarifa ikifika makwao kuwa wanafungwa na kupewa adhabu
kali ndipo wataacha kuingia nchini kwani watajua Tanzania sio mahala pa
mchezo wala kukimbilia.
“Hii
kuwakamata kuwapiga faini na kuwarudisha kwao ndio maana wanafanya
mchezo mchezo kukimbilia huku,ukiwapiga faini wanakwenda wanarudi ni
mchezo wa kuigiza”alisema .
Kamanda
Shanna alielezea kwamba,Tanzania ina sheria zake endapo sheria
zitawabana wahamiaji hao na kukoma kugeuza nchi kuwa lango lao la kupita
kwenda nchi jirani ikiwemo Afrika ya kusini.
Hata
hivyo ,kamanda huyo alisema wahamiaji waliokamatwa wameshawafikisha
ofisi ya uhamiaji mkoani hapo na watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma
zinazowakabili.
Jeshi
hilo,linaendelea kudhibiti wahamiaji haramu ili kupungua wimbi kubwa
linaloingia kupitia njia za panya mkoani hapo hasa bandari bubu 18
zilizopo Bagamoyo .
Pamoja na hilo,Kamanda Shanna alisema wanafanya oparesheni kusaka wahalifu mbalimbali ,zoezi ambalo ni endelevu.
No comments:
Post a Comment