Baraza
la Habari Tanzania (MCT) limezindua Ripoti ya Hali ya Vyombo vya Habari
hapa nchini kwa mwaka 2016 (State of the Media Report) ambapo ripoti
hiyo hutolewa kila mwaka ili kuushirikisha umma
Pia
Baraza hilo linatoa ripoti kuhusu kuvamiwa kwa Studio za Clouds Media
na kubaini jinsi tukio hilo lilivyoathiri uhuru wa vyombo vya habari na
uhuru wa uhariri.
Akizungumza
na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Katibu wa Baraza hilo amesema
ripoti hiyo haina lengo baya, bali ni kuweka bayana hali ya tasnia ya
habari na kwamba hambo hilo si mara ya kwanza kwani baraza hilo limekuwa
likitoa ripoti kama hizo kila mwaka.
“Hatujafanya
uchunguzi huu kwa kuwa tuna mapenzi na Clouds Media wala kwa sababu
tuna mahusiano na Mkuu wa Mkoa, badala yake tumetoa ripoti hii kwa
mujibu wa katiba ya MCT,” alisema katibu.
No comments:
Post a Comment