Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imesema kuwa imeamua
kushirikisha taasisi zingine za kimataifa ili kuwachunguza baadhi ya
watuhumiwa wa Escrow kama wamehifadhi fedha nje ya nchi.
Hayo
yamesemwa na Afisa Habari na Uhusiano wa taasisi hiyo, Mussa Misalaba
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam,
ambapo amesema kuwa watuhumiwa wote wa Escrow bado wanaendelea
kuchunguzwa.
Amesema
kuwa Takukuru inaendelea kuwachunguza watuhmiwa wote huku ikishirikiana
na baadhi ya taasisi za nje na kwamba uchunguzi huo unafanyika kwa
umakini zaidi ili haki itendeke.
“Hili
jambo linafanyika kwa umakini mkubwa, usione kimya kuna jambo
linafanyika, kwa sasa ni mapema sana kusema chochote kuhusu jambo hili
kwakuwa linahitautlivu mkubwa kulishughulikia,”amesema Misalaba
Aidha,
hivi karibuni TAKUKURU iliwafikisha mahakamani baadhi ya watuhumiwa wa
ufisadi na uhujumu uchumi ili kujibu mashtaka yanayowakabili.
Waliofikishwa
mahakamani kujibu tuhuma ni pamoja na Theofilo Bwakea, Mkurugenzi wa
Kampuni ya VIP Engineering and Markerting, na aliyekuwa Mkurugenzi wa
Kampuni ya IPTL, James Rugemalila wote wakikabiliwa kesi ya uhujumu
uchumi
No comments:
Post a Comment