Kiongozi
wa Muungano wa Vyama vya Siasa Nchini Kenya (NASA), Raila Odinga
amewashauri wafuasi wake kutoingia ofisini kuanzia leo jumatatu ili
kuonyesha shinikizo la kutokubaliana na matokeo ya uchaguzi mkuu
uliofanyika hivi karibuni.
Ameyasema
hayo jana wakati akihutubia wafuasi wake jijini Nairobi kwa mara ya
kwanza tangu kutangazwa kwa matokeo, ambapo Rais Uhuru Kenyatta
alitangazwa mshindi kitu ambacho kilipingwa vikali na Odinga.
Aidha
Odinga alisema kuwa siku ya Jumanne, muungano wa vyama hivyo utatoa
msimamo wake kuhusu mwelekeo watakaouchukua kulingana na kutokubaliana
na matokeo hayo kwa madai kuwa yamechakachuliwa.
Rais
Uhuru Kenyatta alitangzwa mashindi kwa kura 8,203,290 huku Raia Odinga
akipata kura 6,762,224 kitu ambacho muungano huo wa vyama vya siasa
unapinga matokeo hayo kwa kusema yamebadilishwa.
Hata
hivyo, Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, ambaye
alikuwa mpatanishi mkuu baada ya mzozo wa kisiasa nchini Kenya miaka
kumi iliyopita, amemshauri Odinga kutumia hatua za kisheria kutafuta
haki kuhusu matokeo ya uchaguzi wa urais kama anaona kaonewa.
No comments:
Post a Comment