Vigogo
6 kati ya 12 wanaotuhumiwa kuhusika kwenye kashifa ya ufisadi wa soko
la Kimataifa la Mwanjelwa jijini Mbeya wamepandishwa kizimbani katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Mbeya na kusomewa mashtaka matatu ya
uhujumu uchumi.
Waliopandishwa
kizimbani Mahakamani hapo ni aliyekuwa Meya wa jiji hilo, Athanas
Kapunga (70) aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji hilo, Elizabeth
Munuo (65) na aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Jiji hilo Dk. Samwel Lazaro
ambaye kwa sasa ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe.
Wengine
ni aliyekuwa Mtunza Hazina wa Jiji hilo, James Jorojik (62), aliyekuwa
Mwasibu wa jiji hilo, Tumaini Msigwa (47) na Mhandisi wa jiji hilo,
Emily Maganga (42).
Mwendesha
mashtaka wa serikali, Shadrack Martin, akisaidiwa na Hebel Kihaka
pamoja na Baraka Mgaya wakati akiwasomea mashtaka yanayowakabili vigogo
hao alisema wote kwa pamoja walitenda makosa ya uhujumi uchumi kati ya
mwaka 2008 na 2013 hivyo kuisababishia serikali hasara kubwa.
Katika
Shtaka la kwanza mwendesha mashtaka huyo alisema linawahusu watuhumiwa
waili ambao ni Athanas Kapunga ambaye alikuwa Meya wa Jiji la Mbeya na
Elizabeth Munuo ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Jiji ambao wanadaiwa
kuisababishia halmashauri hiyo hasara ya Shilingi Bilioni 3.3, ambapo
wanadaiwa kusaini mkopo wa kiasi hicho cha fedha kutoka katika Benki ya
CRDB ambao ulianza kulipiwa riba kabla ya kuanza kujengwa kwa Soko hilo
la Mwanjelwa kinyume cha vifungu vya sheria namba 57 (1) na 60 (1) na
(2) vya Sheria za uhujumu uchumi Sura ya 200 ya mwaka 2002.
Martini
alisema shtaka la pili linawahusu Dk.Samwel Lazaro, James Jorojik,
tumain Msigwa na Emily Maganga ambao kwa pamoja wanadaiwa kushindwa
kutekeleza majukumu yao kwa kuidhinisha malipo ya shilingi milioni
304,470,500 kwa Mkandarasi aliyekuwa anajenga soko hilo, Nandhra
Engineering and Constaction ltd wakati kazi hiyo ilikuwa tayari
imefanywa na Kampuni ya Tanzania Building Works ltd.
Aidha
Washtakiwa wa Shataka namba mbili pia wanashtakiwa kwa kosa la tatu la
kuisababishia Halmashauri ya Jiji hasara ya shilingi 1,140,228,750 kwa
kuidhinisha malipo ya fedha hizo kwa wakandarasi Tanzania Building Works
na Nadhra Engineering kwa ajili ya ujenzi wa Soko hilo wakati kazi
iliyotajwa haikuwemo kwenye Mkataba.
Washtakiwa
hao kwa pamoja walikuwa wakitetewa na Mawakili watatu wakiongozwa na
James Kyando, Baraka Mbwilo na Secilia Luhanga ambao waliiomba Mahakama
hiyo kutoa maelezo kuhusu uwezekano wa wateja wao kupata dhamana. H
ata
hivyo Mwendesha Mashtaka wa serikali alisema upelelezi wa shauri hilo
bado haujakamilika hivyo akaiomba mahakama kupanga siku nyingine kwa
ajili ya kutajwa tena.
Hakimu
Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mbeya, Michael Mteite alisema
Mahakama haina uwezo wa kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi hivyo
washtakiwa wataendelea kukaa mahabusu hadi Agosti 29, Mwaka huu kesi
hiyo itakapotajwa tena.
Kufikishwa
Mahakamani kwa vigogo hao kunatokana na agizo la Waziri mkuu alilotoa
Julai 31 mwaka huu wakati wa ziara ya kikazi jijini hapa alipozungumza
na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya na Jiji na kuwataja
wahusika 13 waliotajwa kwenye Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali (CAG) na kupendekeza wachukuliwe hatua.
No comments:
Post a Comment