Kituo cha Sheria na haki za Binadamu (LHRC) kimelaani vikali vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu vinavyoendelea nchini.
Pia wamelaani kitendo cha Wakala wa barabara nchini (Tanroads) kuidharau mahakama na kuminywa kwa haki za wanasiasa.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Hellen
Kijo-Bisimba amesema wameshangazwa na uamuzi wa Tanroads wa kubomoa
nyumba za wananchi wa Kimara hadi Kiluvya wakati wanapingamizi la
Mahakama.
"Tunalaani
kitendo hiki na tunaona ilichofanya Tanroads ni kuidharau Mahakama
ambapo kwa lugha ya kisheria tunaita Contempt of Court(kuiingilia
Mahakama) "amesema
Mkurugenzi
huyo pia amesema wanalaani kitendo cha kukamatwa ovyo kwa wanasiasa na
kusema kitendo hicho ni kuminywa kwa haki za kisiasa.
"Hali hii imejitokeza sana kwa kuwanyanyasa wabunge wa vyama vya upinzani bila kufuata misingi ya kisheria na haki za binadamu "amesema
Amesema
ukamatwaji wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mbunge wa
Bunda mjini Ester Bulaya aliyekamatwa akiwa hotelini kwa tuhuma za
kutaka kuhudhuria mkutano nje ya jimbo lake na kudai kuwa huo ni
ukiukwaji wa haki na kunyimwa uhuru wa vyama vya upinzani kufanya kazi
yake.
No comments:
Post a Comment