Na Derick LWASYE
Mbeya city wameendelea kupata shida kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini hapa baada ya kulazimishwa sare ya kuto kufungana na Stand united ya Shinyanga.
Mchezo huo uliyotawaliwa na rafu za hapa na pale kutoka kwa timu zote,ulishudiwa safu za ushambuliaji za timu zote kukosa umakini katika ukwamishaji wa mpira Nyavuni.
Baada ya kumalizika kwa mchezo huo makocha wa timu zote mbili walizungumzia mchezo huo,kocha wa Mbeya city Ramadhan Nsanzurwimo amesema walijipanga kuibuka na pointi tatu ila ubora wa Stand united hasa sehemu ya ulinzi ndiyo ulikuwa kikwazo kwa timu yake kuibuka na ushindi.
Naye Athuman Bilal ambaye ni kocha wa Stand united amesema kuwa wao walikuwa wamejipanga kupata pointi tatu ila hata hiyo pointi moja kwao ni muhimu maana walikuwa ugenini.
"Tulijipanga kuondoka na pointi tatu ila hata hii moja siyo mbaya maana kupata pointi moja ugenini si haba" alisema Bilal.
Kesho jumatatu kutakuwa na mchezo mwingine kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini hapa kati ya Tanzania Prisons dhidi ya Mwadui fc majira ya saa kumi jioni.
No comments:
Post a Comment