SE 4 EP 1 HADI YA 5 TAYARI IMESHATOKA JIPATIA EPISODI HIZI KATIKA INBOX YAKO KWA SH 100 TU KWA EP MOJA.
MTOTO WA MTAA SE 3 EP 36
ILIPOISHIA….
“sikujua kwamba ..”
“hukujua nini mzee kahena , tayari ulikwishaonywa kwamba hapa sio sehemu sa hihi, lakini ubinafsi wako ndio umesababisha yote haya, unajua nini sasa hivindio nimeanza kuelewa kwa nini ulikaa mbali na mimi kwa kipindi chote hicho .”
Aliongea Emily kwa kufoka.
MUENDELEZO WAKE:
Hospitali ya Aga khan iligeuka uwanja wa vita , watu walikimbia hovyo hovyo , wengine walikuwa wagonjwa mahututi lakini mara baada ya kusikia milio ya risasi walipona na kukimbia kama vile ni wazima wa afya , wauguzi madaktari nao pia walishindwa kufanya kazi zao badala ya wao kuwa saidia wagonjwa kwa kuwazuia wasikimbie wao ndio walikuwa mstari wa mbele kuacha wagonjwa vitandani.
Kwa kweli hakuna aliyejua nini hasa kiliendelea, hata uongozi wa hospitalui haukuwa na taarifa juu ya kuingia kwa askari hao hapo, walifika tu na kuanza msako wao kiholela .
“ni nini hiki mbona sielewi ni magaidi wameteka hospitali?”
Aliuliza mganga mkuu mara baada ya kutoka ofisini kwake kwa kukurupuka.
“hapana mheshimiwa kikosi maalumu cha askari , wanamsaka jambazi sugu.”
Mmoja kati ya watabibu alimjibu.
“askari , kwa nini wanafanya mambo kiholela hivi jamani , hawajui kwamba wana hatarisha maisha ya wagonjwa?”
Aliongea mganga mkuu.
“hata mimi sielewi mheshimiwa , wame ingia kwa vurugu na kusema hawana muda wa chochote na muda kidogo tu wakaanza kutupa risasi hovyo.”
“Mungu wangu hawa watu mbona wanataka kuleta maafa .”
Aliongeas mganga huyo na kutoka nje , hakujali milio hiyo iliyosikika bali alisogea kule kule milio hiyo ilikotokea.
‘unafanya nini mheshimiwa?’
“natakiwa kuwazuia , hii ni hospitali , sio uwanja wa vita hawawezi , kuwatenda hivi wa gonjwa .”
Aliongea daktari huyo na kuendelea kusonga mbele kuelekea katika chumba cha upasuaji.
Risasi mfululizo zilikuwa zikitupwa kwenye chumba hicho , deo akiwa amejibanza kwenye moja kati ya korido za chumba hicho.
Hakuwa na siraha yoyote ya kujibu mashambulizi , wala hakuwa na namna yoyote ya kutoka ndani ya chumba hicho , askari hao walikuwa wamekizunguka chumba chote na kutupa risasi hovyo , hawakujali humo kuna mgonjwa , wauguzi au daktarei , ni kwa bahati tu chumba hichio hakikuwa na mgonjwa yoyote na kilisimamishwa kutumika kwa sababu ya matengenezo fulani , hivyo upasuaji ulifanyika kwenye chumba kingine cha dharula , la sivyo sijui hata ingekuwaje.
“acheni , acheni , Muogopeni mungu nyie , hapa ni hospitali jamani , nyie ni askari wa aina gani? mnataka kupoteza mamia ya roho za watanzania sababu ya mtu mmoja?”
Aliongea mganga mkuu mara baada ya kuwafikia askari hao.
Embu kaa pembeni daktari , hiki ni kikosi maalumu , tunachofanya sisi ni kufuata amri toka kwa mkuu wetu wa kazi na si mtu yoyote.”
Aliongea askari huyo na kumsukuma mganga huko , kisha kuushika vema mtutu wake na risasi zikaendelea kumimi nika.
Askari hawa walikuwa na uhakika kwamba huu ndio utakuwa mwisho wa maisha ya deo , tangu waaanze kumsaka leo ndio siku waliokuwa wamemuweka kwenye sehemu ngumu zaidi.
Emily alikuwa akilia muda wote akiwa amekumbatiwa na baba yake ambaye alikuwa akimbembneleaza kinguvu , kila akijaribu kumpokonyokaa mzee huyo emily alishindwa kwa sababu alikuwa amemshikilia kisawa sawa.
“najua unaumia mwanangu , lakini siwezi kukuacha na fahamu kwamba utaenda kufanya kitu cha kijinga, nikikuachia.”
Aliongea mzee kahena huku akiwa amembana Emily .
“niachie , niachie mimi , niache nikafe na deo wangu.’
alilia emily huku akiendelea kujaribu kujipokonyoa mwilini mwa baba yake.
Deo ndani ya chumba hicho alikuwa amelala sakafuni huku vumbi lakuta zilizokuwa zikutupiwa risasi likimdondokea .
“acheni , acheni ,acheni kutupa risasi, nafikiri sasa atakuwa amekwisha .’
Aliongea askari huyo na kuonyesha ishara kwa askari kadhaa iliyowataka waingie ndani ya jengo hilo kukagua . lakini kabla ya kufanya hivyo askari hao walivaa vifaa maaalumu vya kupumulia na na kisha wakatupia bomu la machozi kwenye chumba hicho.
Lengo lao lilikuwa ni kumkuta deo akiwa hoi hajitambui kwa lolote , ili wasipate tabu kumvamia na kumfyatulia risasi kama ilivyo amri waliyopewa.
Deo alililiona bomu hilo , alijaribu kujizuia kwa kujifunika uso wake kwa shati alilovaa , huku akijikaza kutopumua kwa muda Fulani lakini pumzi yake haikuweza kudumu kwa muda mrefu kiasi hicho alijikuta anashindwa kujizuia na gesi hiyo, mwili wake ulilegea akawa hoi kabisa ,
” ingia , ingia haraka , huu ndio muda muhafaka”
Aliongea kiongozi wa askari hao utafikiri alikuwa anamuona deo jinsi alivyokuwa amenyong’onyea ndani ya chumba hicho. Askari hao waliingia ndani ya chumba hicho na kupiga hatua taratibu, mpaka wakamfikia deo akiwa amelala chini ajitambui, kitu pekee kilichosikika hapo ni mlio wa mshale wa saaa iliyokuwa imedondoka chini, na kulia ta t a ta , ghafla mlio huo ulimezwa na mlio wa risasi mfululizo zilizomiminika . Hakuwa deo wala askari hao bali mtu mwingine na tena alizifyatua risasi hizo toka mbali na kusababisha askari hao washindwe hata kupiga hatua moja kusogelea alipokuwa amelala deo , kuna wengine walipatwa na risasi hizo na kufa hapo hapo.
Kilichotokea hapo hakuna aliyekuwa amekitegemea , askari hao walisogea nyuma na kujibanza wakiwa hawaelewi hili wala lile , risasi zaidi zilitupwa , waligundua kwamba mtu aliyetupa risasi hizo alikuwa ni sniper , mahali aliposimama sniper huyopo hakuna aliyejua , wakiwa hawelewi hil li wala lile kwa ghafla walisikia muungurumo wa gari likija kwa kasi huku likitupa risasi kuelekea hapo walipo , askari waliokuwa pale nje walipatwa na risasi hizo n a wakajikuta wakianguka mmoja baada ya mwingine wengine walikimbia na kujificha katika mahodi ya wagonjwa. Japo watu hao hawakujali walitupa risasi piopote askari hao walipoelekea. Walifanya vurufgu hizo huku wakishangilia hawakuwa wenginer bali ni John na watu wake .
Walipata taarifa juu ya kuvamiwa kwa deo katiaka hospityali hiyo toka kwa shushu wao na sasa walikuwa wamejipanga kwa ajili ya kumuokoa , hawakujali kwamba deo alikataa kata kata kuwa pamoja nao , bado walikuwa na tumaini nae , safari hii kikosi cho kilikuwa kimeimarika zaidi , watu wote wa mbututu walikuja kuungana nao , pamoja na kuwa kikosi kikubw achenye nguvu lakini bado hawakujiona wamekamilika bila ya deo , walimuhitaji kwa gharama yoyote ile .
Mpaka wanafika katika chumba hicho cha upasuaji hakuna hata askari mmoja aliyekuwa hai akizengea zengea katika eneo hilo , wajanja walishatimua mbio kitambo , kupotea kabisa katika eneo hilo , waliiingia katika chumba hicghopo john aklimuinua deo na kumtoa katika chumba hichop, daktari aliitwa haraka na kuamrishwa kumhudumia , alipewa huduma ilityomfanya arejee katika hali yake , kisha waskatoka nae hospitalini hapo haraka
“unanipeleka wapi john? nimeshakueleza mimi siwezi kufanya kazi tena.”
“afya yako bado haijatulia Deo unahitaji kuwa mahali salama kwa muda .”
Aliongea john. Alimjua deo aking’ang’ania kitu , muda huo hakutaka waanze kubishana , gari liliendelea kusonga mbele bado walikuwa katyika Barbara ya obama, japo walikuwa wanaelekea kuchepuka.
Hakuna gari ya polisi iliyowafuata, bali walipisha na nayo yakienda kwa kasi katika eneo la tukiop wakiwa wamejaza vikosi, kwa ajili ya kwenda kuendesha oparesheni ya kupasmbana na majambazi bila kujua kwamba majambazi ndio hao wanaopishana nao.
Itaendelea…
MTOTO WA MTAA SE 3 INAKWISHA LEO EPISODI YA 65 HADI 70 IMESHAKAMILIKA JIPATIE EPISODI HIZI KATIKA INBOX YAKO YA FB AU WHATSAP BEI NI ILE ILE SH 100 TU KWA EPISODI NAUZA UKUANZIA EPISODI SITA KWA WALE WALIOBAKIZA EPISODI ZA MWISHO NA KUANZIA EPISODI 10 KWA MNUNUZI MPYA.
Namba zinazotumika kwa ajili ya malipo ni mpesa 0757 414 436 , tigo pesa 0715 557 191 airtel money 0789 117 674
Namba zote zimesajiliwa kwa jina la Deogratius Lwasye

No comments:
Post a Comment