Tuesday 20 March 2018

KIMBIA MPENZI TUTAKUTANA MBELE KWA MBELE!!(Sehemu ya 8)


                                                    (the first run away love to told by Deogratius gift kipapa.)
EPISODI 08
INTRO:
Simulizi ya msichana wa shule aliyelazimika kumtorosha mpenzi wake mbali na baba yake pamoja na serikali mara baada ya kumpa ujauzito. Kamwe hakufikiri kwamba kumruhusu akimbie ni kuliruhusu penzi lake lipotelee mbali milele.  Simulizi hii, haitakuonyesha ni jinsi gani ilivyo kutengana na mpenzi wako pekee bali pia itakushangaza zaidi na uhusiano wa baba na mwana ambao kamwe hukuwahi kuuvutia picha, kuna machozi, na jasho, mbio na kuvuta pumzi, kama ulisoma simulizi yoyote ya mapenzi kutoka kwa gift kipapa na kuhakikishia ya kwamba haujasoma kitu. This is not just a heart to heart story but I run away love which no one could never ever found.
ILIPOISHIA EPISODI 7….
“mamaaa, maamama , gari linaondoka.”
Aliongea mtoto huyo mara baada ya gari hilo kuanza safari.
“tulia wewe.’
Aliongea mama yake kwa ukali.
Basi hilo lilikuwa limefikia geti la kutokea katika stendi hiyo.
Maana yake safari ya kuuaga mji wa mbeya ndio ilikuwa inaanza rasmi, kila kitu kilikuwa kigeni kwa wakati ndani ya nusu saa , zile nyumba na makazi ya watu aliyoendelea aliyokuwa anayaona wakati basi hilo lilipo kuwa ndani ya mji wa mbeya vyote vilipotea ,  alichokiona kwa muda  huo yalikuwa nyumba moja moja zilizojitenga  na hii miti iliyokuwa kando ya bara bara iliyokuwa inarudi nyuma kwa kasi pamoja na milima na mambonde ambavyo vyote vilikuwa vikimshangaza kupita kiasi.
***
“ni wakati ! ni wakati!”
Aliongea pendo kwa woga huku akilia , muonekano wa baba yake ulikuwa ukimtisha kupita kiasi .
“wakati ? , wakati ndio nani?”
Aliuliza mzee fanuel kwa mshangao, kusema kweli alimjua wakati fika lakini kichwani kwake hakuwa mtu anayeweza kumfikiria kwa namna yoyote ile.
“yule mchoma kitimoto kule njia panda ya shule.”
Aliongea pendo huku akizidi kutetemeka , alijua akisema hivyo atamfanya baba yake akasirike zaidi .
“hapana , hapana , hawezi kuwa yeye , huwezi kunidharirisha kiasi hiki mwanangu , mimi ni daktari , mwanangu huwezi kudanganyika kwa vipande vya nyama , haiwezekani.’
Aliongea mzee fanuel akiwa amepagawa kabisa .
“ni yeye baba najua ni meku..”
“nyamaza , nyamaza pendo , huwezi kuniambia ni yeye huwezi .”
Alifoka baba yake na safari hii uso wake ulikuwa umebadilika kabisa alikuwa mnyama , tena mnya ma aliye tayari kumuumiza yoyote kwa kumrarua rarua , hilo lilimfanya pendo azidi kutetemeka kwa hofu .
Hakuongea na yoyote bali kutoka hapo sebuleni kuelekea stoo.
“fanuel hapana! Huwezi kufanya kile unachokifikiria , fanuel tafadhari nisikilize mkeo.”
Aliongea mama yake pendo akijaribu kumzuia lakini hilo lilikuwa jambo lisilowezekana mikono yake tayari ilikuwa imeshalishika panga na alitoka katika stoo hiyo kwa hasira huku akimsukumia mkewe kule.
Kwa kweli alikuwa nje ya akili yake , alikuwa tayari kulitumia vyovyote panga hilo mwilini kwa Wakati , iwe kumcharanga charanga , au kumchinja shingo yake avuje damu mpaka kufa na pengine hapo roho yake itaweza kutulia.
“fanuel hapana , fanuel rudi baba yangu , unakwenda kuiingiza familia yako yote katika matatizo, fanuel mume wangu!”
Mke wake alililia akimsihi arudi , macho yake yalikuwa yamejaa machozi tupu , alimjua mumewe akiwa katika hali hiyo anaweza kufanya lolote .
Pendo alikuwa kimya pale chini akiendelea kulia kwa kuguna guna , pasipo kuhofia kile baba yake anachokwenda kufanya alijua kwamba hakuna anacho kwenda kukutana nacho huko anakoelekea zaidi ya chumba kitupu.
Alifika kwenye nyumba hiyo huku akiwa amejaa hasira tupu , aliangalia kulia mhali na kuvalangua kila kilichokuwemo humo , kitanda alikituopa kule na kukifanya kigawanyike kila muanzi upande wake kamba iliyokuwa imefungwa kuishikiza mianzi hiyo haikufaa tena mikeka ndio aliirusha hovyo mara huku mara kule huku akiirarua rarua kwa panga lake. Alijua kwamba hakuna mtu humo lakini alitaka muda wowote atakapo rejea humo ajue kwamba yuko kwenye matatizo , na pale alipoangalia ukutani ndio hasira zilipo mjaa mara mbili zaidi , kulikuwa na karatasi gumu aina ya manira lilikuwa limebandikwa kwenye ukuta wa chumba hicho likiwa limechorwa mchoro mkubwa wa moyo , huku maneno yaliyoandikwa
“P and W are forever.” Zilikuwa ni herufi za majina yao na maneno ya kingereza yalikuwa na maana kwamba upendo wao ni wa milele.
Mzee fanuel kwa kweli alizidi kupagawa kwa hasira , alikuwa analikumbuyka karatasi hilo vizuri , lilikuwa lake na alimpa pendo, siku moja alipokuja ofisini mwake na kumuomba karatasi kwa ajili ya kuchorea mchoro wa moyo , alisema ni mradi ambao mwalimu aliwaagiza kila mmoja achore moyo wa binadamu jinsi unavyofaya kazi pamoja na mishipa yote inayoingiza na kutoa damu katika moyo , ni kweli alichora moyo lakini huu ulikuwa moyo ule wa mapendo aina ya kopa lavu na haiukuwa mradi wa shuleni bali mradi wa mapenzi.
“aahhhh!  Aaahhh!”
Mzee alipiga kelele kwa hasira huku akiivuta karatasi hiyo na kuichana chana kwa mikono yake.
“Wakati  popote ulipo wewe ni mtu mfu!!”
Aliongea mzee fanuel kwa hasira huku akiupiga ukuta wa kibanda hicho uliosilibwa kwa udongo  juu ya miti iliyopangwa kwa mpangilio mzuri, kibanda chote kilikuwa kikitikisika  na ni kama vile alikuwa anakwenda kukidondosha chini kwa ngumi zake hizo nzito.
Hakuna aliyemzuia  na hasira zake zilizidi kupanda zaidi na zaidi , kama yoyote yule angemkuta hapo asingeweza kufikiria kwamba mwanaume huyo ni daktari bingwa wa upasuaji wa macho , kwa kweli kila kitu hapo alikifanya kama vile mtu ambae hakulionja darasa hata moja .
Miti ya kibanda hicho ilivutana vutana , huku udongo uliokuwa umeishika miti hiyo pamoja na kamba vikidondoka chini , na kilicho fuata hapo ulikuwa mti mmoja mmoja kudondoka na baadae mianzi ya iliyolishikilia paa la nyasi yote ilidondoka , na mzee fanuel alitoka nje ya kibanda hicho huku akiyatupa tupa majani yaliyokuwa yamemzunguka mwilini mwake na kuyasukuma sukuma kwa panga lake, aliichukua bara bara na safari hii alikuwa anaelekea njia panda ya lufilyo  na huko alikuwa ana uhakika wa kukata miguu ya mtu, shingo yake kiuno chake au chochote lakini alihitaji mvulana huyo afe siku hiyo tena afe huku akiishuhudia damu yake ikivuja hadi tone la mwisho.
Itaendelea kesho, pia unaweza kusoma stori sehemu ya mbele ya stori hii zaidi ya episodi 50 zipo tayari, pia unaweza kujipatia vitabu vyetu vingine kwa bei ya nafuu, kuna ofa ya vitabu kwa whatsap na inbox fb, viwili sh 1700 vitatu sh 2400
vinne sh 3200 vitano sh 4000,kimoja sh 1000.
Stori zetu zingine ni hizi zifuatazo:
NOT YOU NOW book 1 – 24 , MTOTO WA MTAA BOOK 1 – 20, I WILL HUNT YOU DOWN 1&2, WHEN I  SAY I LOVE 1 – 9, KIMBIA MPENZI BOOK 1,2,3,4,5 NA 6.  YOU CAN’T MAKE ME A FOOL AGAIN, SISTAHILI KUFUNGWA, NAIPENDA TANZANIA.
BABA WA KAMBO book01,
CHANGUO NGUO book01,02,03
TEKETEKE TAMU BOOK 01,02
YES BOSS BOOK 1,2, ASMA KIDOTI book 1,2,3 MSICHANA NYUMBA YA PILI BOOK1,2, KOCHA WA TENESI BOOK1,2, PITISHA KWENYE  MPASUO, WEZELE,
TWAMTOA MWARI book 1,2,
MCHEPUKO WA MSHUA, KITAA FLANI, MSAGAJI,
TAXI BUBU,
MAMA WA KAMBO BOOK 1,2,
DEMU WA GEREJI, MZEE WA CHUMVINI,
NATAKA ZOTE,
NIPE UTAMU KAKA JAMBAZI,
zamu zamu, OPARESHENI MAPENZI BOOK 1,2 JIRANI NYAMA YA HAMU BOOOK 1,2,3,4,5,6,7 NJOO MAMA HAYUPO 1,2,3,4,5,6 NATAKA UNIFUATE KICHAKANI BOOK 1,2,3,4,5 AISHA CHA UTAMU BOOK 1,2,3,4,5 KIDOLE AKINITOSHI BOOK 1,2,3  BEKI TATU WA MTAA BOOK 1,2,3,4
THE AFRICAN SEX MASHINE BOOK 1,2,3,4,5 na 6 KARIBU KITAA TICHA BOOK 
1,2,3,4,5 , KWAYA MASTA BOOK 1 , 2, 3 na 4 WIFI NIPE UTAMU … KAKA HAYUPO BOOK 1,2&3,4,5,6,7,  SHUGA MUMY LA 
KITASHA BOOK 1,2,3. MUUZA MAZIWA BOOK 1- 16, TOTO LA KISHUA 1- 9, SI UNA MATE NIMEKUSIA BOOK 1 – 5, HALO HALO 1-9, JIMAMA MTAA WA PILI 1 -8,
Namba zinazotumika kwa ajili ya malipo ni mpesa 0757 414 436 , tigo pesa 0715 557 191 airtel money 0789117674
Namba zote zimesajiliwa kwa jina la Deogratius Lwasye.

No comments: