Thursday, 22 March 2018

KIMBIA MPENZI TUTAKUTANA MBELE KWA MBELE!!(Sehemu 9)


                                                    (the first run away love to told by Deogratius gift kipapa.)
EPISODI 09
INTRO:
Simulizi ya msichana wa shule aliyelazimika kumtorosha mpenzi wake mbali na baba yake pamoja na serikali mara baada ya kumpa ujauzito. Kamwe hakufikiri kwamba kumruhusu akimbie ni kuliruhusu penzi lake lipotelee mbali milele.  Simulizi hii, haitakuonyesha ni jinsi gani ilivyo kutengana na mpenzi wako pekee bali pia itakushangaza zaidi na uhusiano wa baba na mwana ambao kamwe hukuwahi kuuvutia picha, kuna machozi, na jasho, mbio na kuvuta pumzi, kama ulisoma simulizi yoyote ya mapenzi kutoka kwa gift kipapa na kuhakikishia ya kwamba haujasoma kitu. This is not just a heart to heart story but I run away love which no one could never ever found.
ILIPOISHIA EPISODI 8….
Miti ya kibanda hicho ilivutana vutana , huku udongo uliokuwa umeishika miti hiyo pamoja na kamba vikidondoka chini , na kilicho fuata hapo ulikuwa mti mmoja mmoja kudondoka na baadae mianzi ya iliyolishikilia paa la nyasi yote ilidondoka , na mzee fanuel alitoka nje ya kibanda hicho huku akiyatupa tupa majani yaliyokuwa yamemzunguka mwilini mwake na kuyasukuma sukuma kwa panga lake, aliichukua bara bara na safari hii alikuwa anaelekea njia panda ya lufilyo  na huko alikuwa ana uhakika wa kukata miguu ya mtu, shingo yake kiuno chake au chochote lakini alihitaji mvulana huyo afe siku hiyo tena afe huku akiishuhudia damu yake ikivuja hadi tone la mwisho.
MWENDELEZO WAKE:
Watu wote waliokuwa kwenye vibanda vya jirani walitoka nje kuangalia shoo hiyo , hawakupiga yowe wala vifijo bali kila mmoja alimshtua mwenzake kwa kukonyezana.
Tangu walipomuona Wakati akimkumbatia Pendo na kuongea nae kimahaba asubuhi ya jana kila mmoja alijua kwamba siku kama hii ingekuja kwake.
Japo hawakutegemea kumuona mzee fanuel akiwa amepagawa kiasi hicho , japo kila mmoja alijua uhusiano wa Wakati na mzee huyo ulikuwa mzuri mno, kila mtu alikuwa akimuonea wivu jinsi ambavyo alikuwa akimuungusha. Na wakati mwingine alikuwa akiongea nae na kutania na nae kama rafiki.
Na kwa mtu aliyemjua vema mzee fanuel ilikuwa kweli kusema wakati alikuwa rafiki yake , alikuwa ni aina ya mwanaume ambae alikuwa hajichanganyi sana na wenzake , yeye alikuwa ni mtu wa nyumbani na ofisini na ukizungumzia kuhusu marafiki wakati wote alikuwa akizunguka na mkewe pamoja na binti yake , walizunguka kila mahali pamoja , iwe kanisani, sokoni au popote, na hilo lilimfanya aonekane mwanaume anayeipenda familia yake kuliko mwanaume yoyote hapo.
Na jambo lililokuwa linashangaza zaidi wakati ndio mvulana pekee aliyekuwa anauwezo wa kuongea na pendo mbele yake , wavulana wengine wote walikuwa wanamuogopa mwanaume huyo kama vile wanaogopa kifo. Na pengine walipaswa kufanya hivyo , walimuona kila hasubuhi akifanya mazoezi huwanjani na wala hakuwa anacheza mpira au kukimbia kama ilivyo kwa kila mmoja , bali yeye alikuwa akicheza kungfu , karate na tai kondo.
Kwa kweli alipaswa kuwa askari jeshi tena yule anayetumwa kwenye misheni za mauaji ya kivita , lakini yeye alikuwa ni daktari tu , alikuwa anajali macho ya kila mmoja .
Na alikuwa akipata tuzo ya udktari bora kila mwaka.
“aahhhhh, aaahhh!”
Ilikuwa ni sauti yake huku panga lake likizipiga piga nguzo za miti ya mianzi zilizokuwa zimekishikilia kipanda hicho na nacho pia kiliishia kama vile kilivyoishia kile kibanda cha makazi ya wakati .
Yani kama kweli wakati bado angekuwa ndani ya mji huo basi, angekuwa hana makazi usiku wa siku hiyo.
***
Yalikuwa ni majira ya saa saba na robo ya  mchana, Basi lilifunga breki yalikuwa ni maeneo ya ililula, mji mdogo uliojengeka kando kando ya bara bara katika mkoa wa iringa ambapo mabasi mbali mbali huwa yanasimama kwa muda kwa ajili ya abiria kupata chakula.
Kila mmoja alishuka kwa ajili ya kuingia kwenye migahawa iliyokuwa kando kando ya bara bara hiyo.
Lakini wakati alibaki , alifungua mkoba wake na kutoa mfuko wa plastiki , ambao Pendo alimpatia.
Alipoanza kuufungua mfuko huo aliiona sura ya pendo kwenye macho yake na masikioni mwake aliisikia sauti yake.
“ chakula usikifungue sasa hivi , nataka mpaka ukiwa ndani ya basi , nataka ule ukiwa unakikumbuka kwamba ndio chakula chako cha mwisho kula kutoka kwangu.”
Sauti hii toka kwa pendo ndio iliyosikika masikioni mwa wakati kwa muda huo na kumfanya aanze kudondosha machozi tena, na pale alipokifungua chakula hicho ndio machozi yaliongezeka, zilikuwa ni chapati na maharage , pendo alikuwa anajua ni jinsi gani wakati alikuwa anakipenda chakula hicho, kwa dakika hiyo kila kitu kiliwa kama kilivyokuwa , yalikuwa maumivu ambayo aliamini kamwe hayatakuja kukoma katika maisha yake, kukaa mbali na pendo lilikuwa ni jambo ambalo alikuwa analiogopa kuliko hata kifo.
Na leo jambo hilo limemtokea  chaguo pekee alilonalo kwa wakati huo ni kukimbia, alijua baba yake pendo kamwe asingeweza kumuangalia kama vile alivyokuwa akimuangalia kwa wakati wote .
Alikumbuka vile alivyokuwa akimuamini , na hata katika msiba wa bibi yake alikumbuka kuuona mkono wake ukilishika bega lake kumfariji, aliahidi kumsaidia japo hakuweka wazi msaada wake utakuwa wa aina gani, japo sasa hivi anaweza kuwa mtu pekee anayemtaka afie mbali au hata kutiwa mbaroni na kuchakaa jera , kwa sababu ameharibu kila kitu walichokijenga katika uhusiano wao.
“lakini nitarudi kwa aajili yako, pendo , haijalishi baba yako atakuwa ananichukia kiasi gani , nitarudi kwa ajili yako nay a mtoto wetu , naahidi.”
Alijisemesha kimoyo moyo huku machozi yakiendelea kumbubujika , abiria zaidi waliingia ndani ya basi wakiwa na vyakula walivyonunua, alipomuona yule mwanamke mwenye mtoto akiingia , wakati alijifuta uso wake haraka , na kuanza kula , alijua huyo mtoto akimkuta analia lazima atakuja na yale maswali yake ya udadisi, najibu lolote ambalo angelijibu ni lazima lingemfanya adondoshe machozi zaidi na hiyo ingekuwa aibu kwake.
“mambo ona! ona, mama ameninunulia kuku!”
Aliongea mtoto huyo mara baada ya kuingia na kuketi na mama yake , mikono yake ilikuwa imelishikilia paja la kuku  alilokuwa ameanza kulitafuna toka huko nje.
“oh , mama mzuri , kuku na nini?”
Aliuliza .
“na chips.”
Aliongea mtoto huyo huku akitabasamu.
“oh safi sana , mwambie ahsante mama.”
“ahsante mama.’
Mtoto huyo aliongea huku akimuangalia mama yake usoni.
Itaendelea kesho, pia unaweza kusoma stori sehemu ya mbele ya stori hii zaidi ya episodi 50 zipo tayari, pia unaweza kujipatia vitabu vyetu vingine kwa bei ya nafuu, kuna ofa ya vitabu kwa whatsap na inbox fb, viwili sh 1700 vitatu sh 2400
vinne sh 3200 vitano sh 4000,kimoja sh 1000.
Stori zetu zingine ni hizi zifuatazo:
NOT YOU NOW book 1 – 24 , MTOTO WA MTAA BOOK 1 – 20, I WILL HUNT YOU DOWN 1&2, WHEN I  SAY I LOVE 1 – 9, KIMBIA MPENZI BOOK 1,2,3,4,5 NA 6.  YOU CAN’T MAKE ME A FOOL AGAIN, SISTAHILI KUFUNGWA, NAIPENDA TANZANIA.
BABA WA KAMBO book01,02,03,
CHANGUO NGUO book01,02,03
TEKETEKE TAMU BOOK 01,02
YES BOSS BOOK 1,2, ASMA KIDOTI book 1,2,3 MSICHANA NYUMBA YA PILI BOOK1,2, KOCHA WA TENESI BOOK1,2, PITISHA KWENYE  MPASUO, WEZELE,
TWAMTOA MWARI book 1,2,
MCHEPUKO WA MSHUA, KITAA FLANI, MSAGAJI,
TAXI BUBU,
MAMA WA KAMBO BOOK 1,2,
DEMU WA GEREJI, MZEE WA CHUMVINI,
NATAKA ZOTE,
NIPE UTAMU KAKA JAMBAZI,
zamu zamu, OPARESHENI MAPENZI BOOK 1,2 JIRANI NYAMA YA HAMU BOOOK 1,2,3,4,5,6,7 NJOO MAMA HAYUPO 1,2,3,4,5,6 NATAKA UNIFUATE KICHAKANI BOOK 1,2,3,4,5 AISHA CHA UTAMU BOOK 1,2,3,4,5 KIDOLE AKINITOSHI BOOK 1,2,3  BEKI TATU WA MTAA BOOK 1,2,3,4
THE AFRICAN SEX MASHINE BOOK 1,2,3,4,5 na 6 KARIBU KITAA TICHA BOOK 
1,2,3,4,5 , KWAYA MASTA BOOK 1 , 2, 3 na 4 WIFI NIPE UTAMU … KAKA HAYUPO BOOK 1,2&3,4,5,6,7,  SHUGA MUMY LA 
KITASHA BOOK 1,2,3. MUUZA MAZIWA BOOK 1- 16, TOTO LA KISHUA 1- 9, SI UNA MATE NIMEKUSIA BOOK 1 – 5, HALO HALO 1-9, JIMAMA MTAA WA PILI 1 -8,
Namba zinazotumika kwa ajili ya malipo ni mpesa 0757 414 436 , tigo pesa 0715 557 191 airtel money 0789117674
Namba zote zimesajiliwa kwa jina la Deogratius Lwasye.

No comments: