Wednesday, 14 March 2018

KIMBIA MPENZI TUTAKUTANA MBELE KWA MBELE!!(Sehemu ya Tano)


                                                    (the first run away love to told by Deogratius gift kipapa.)
EPISODI 05
INTRO:
Simulizi ya msichana wa shule aliyelazimika kumtorosha mpenzi wake mbali na baba yake pamoja na serikali mara baada ya kumpa ujauzito. Kamwe hakufikiri kwamba kumruhusu akimbie ni kuliruhusu penzi lake lipotelee mbali milele.  Simulizi hii, haitakuonyesha ni jinsi gani ilivyo kutengana na mpenzi wako pekee bali pia itakushangaza zaidi na uhusiano wa baba na mwana ambao kamwe hukuwahi kuuvutia picha, kuna machozi, na jasho, mbio na kuvuta pumzi, kama ulisoma simulizi yoyote ya mapenzi kutoka kwa gift kipapa na kuhakikishia ya kwamba haujasoma kitu. This is not just a heart to heart story but I run away love which no one could never ever found.
ILIPOISHIA EPISODI 04….
Iliwachukua muda kidogo kuufikia mji wa lwangwa , ulikuwa ni mji mdogo lakini ulikuwa na kelele na vurugu za kila aina katika soko lake ambalo lilikuwa limejaa bidhaa za kila aina.
Wakulima wa ndizi walikuwa wamesimama nyuma ya mikungu yao na kumuita yoyote Aliyepita karibu yao ili anunue japo hata kichanja kimoja cha mkungu huo .
Sehemu ya matunda hali nayo ilikuwa hivyo hivyo maparachichi, maembe yalikuwa yamejaa kwenye meza , na wauzaji walikuwa wakipiga kelele muda wote kumuita yoyote.
Wakati pamoja na pendo walitakiwa kupita kati kati yao, walivutwa mkono na baadhi ya wauzaji hao waliokuwa wakisisitiza kununuliwa kwa bidhaa zao , lakini walibaki kimya.
Angalia , wakati , basi la sikutegemea! na tena limebaki peke yake.”
Aliongea pendo huku akionyesha basi kubwa lililokuwa lkimeegeshwa kwenye stendi ya mji huo likiwa na maandishi makubwa yaliyoandikwa ‘sikutegemea trans’  kwenye ubavu wake.
MWENDELEZO WAKE:
E5
“nafikiri tuna bahati .”
Aliongea wakati na wakalisogelea basi hilo mpaka lilipokuwa limeegeshwa, walikuta viti kadhaa vikiwa tupu, hiyo ilikuwa na maana bado kuna masaa kadhaa ya kusubiri mpaka gari hilo litakapo anza safari , hilo liliwafanya wakae wote ndani ya basi hilo katika kiti cha nyuma ambacho kilikuwa kimejitenga na abiria wote.

Waliongea kuhusu maisha yao muda wote kila mmoja alikuwa akiongea vile alivyokuwa akiombea kila kitu kiwe pale mambo yatakapotulia.
Pendo alikuwa na silimia zote kwamba mambo yatatulia tu na baba yake atampeleka shule nyingine nzuri kuliko hata ile ya mwanzo , na alimuhakikishia wakati kwamba anatakiwa kukaa huko kwa miaka michache tu na pale kila kitu kitakapoisha arejeee na kuendelea na maisha yao kama ilivyokuwa hapo awali.
“ninaamini kila kitu kitakuwa sawa , wakati , nitakuwa nimemaliza form 4 na mtoto wetu atakuwa ameshaanza kutembea , utakuwa na furaha ya kuwa baba huku tukifurahia kwa pamoja mafanikio yangu katika mtihani wangu wa kidato cha nne.”
Aliongea pendo , na wakati alitabasamu , kwa kweli kila kitu alichokipanga pendo kizuri, toka siku ya kwanza , tangu siku ya kwanza wakati alipokutana nae alijua kwamba amempata msichana wa nguvu, yeye ndio aliyekuja na kumpa hili wazo la kumiliki hoteli jambo ambalo hakuwahi kuwa nalo kabla ya kukutana nae, kitu pekee alichokijua yeye ilikuwa ni kupata pesa na kutimiza mahitaji yake pamoja na bibi na huo ndio ulikuwa mwisho.
“lakini nitakukumbuka , pendo , kwa muda wote huo , kutakuwa hakuna mtu atakaye niambia nifanye nini tena, nitakuwa peke yangu kabisa.”
Aliongea wakati huku akilia.
“hapana wakati , usilie mpenzi wangu , ninaweza kuwa niko mbali , lakini nimeshaongea na wewe mambo mengi tayari , unajua jinsi ya kutunza pesa , bado una ndoto ile ile tuliokuwa nayo pamoja kila kitu kitakuwa sawa , mpenzi , niahidi utarejea kila kitu kitakapo tulia, hilo ndio jambo pekee unalo lihitaji kwa sasa.”
Aliongea pendo.
“nakuahidi, nakuahidi mpenzi wangu, nitakuwa hapa , nitarejea kwa ajili yako na mtoto wetu na tutakuwa na furaha moja ya ajabu.”
Aliongea wakati , lakini macho yake bado yalikuwa yakidondosha machozi, Alichokuwa anakitaka kwa wakati huo kilikuwa kimepita kiasi bado alikuwa amekataa kukubali kila kitu na alikuwa na tumaini ya kufanya ndoto kila kitu , alijaribu kufumba macho yake na kufungua akidhani ataamka na kila kitu kitarudi kuwa kama awali.
“nakupenda wakati , unatakiwa uliweke hilo kichwani mwako.”
Aliongea pendo huku akisisitiza na kumuangalia wakati usoni.
“najua mpenzi , na nakuahidi kupigana kwa ajili ya penzi letu daima.”
Aliongea wakati huku nae pia akimuangalia usoni.
Watu walizidi kuongezeka katika basi hilo mpaka ukafika wakati kiti alichokuwa amekalia pendo ndio kilichobaki.
“natakiwa kushuka wakati , konda anaweza kufikiri na mimi ni abiria.”
Aliongea pendo huku akisimama kwenye kiti hicho , mikono yake bado ilikuwa imeshikwa na wakati , alikuwa anataka aendelee kubaki .
Lakini pale alipoisikia honi ya gari , alijua ya kwamba kila kitu kimefikia mwisho , gari hilo linatakiwa kuondoka sekunde chache tokea hapo, na anatakiwa kumuacha aondoke.
Alipoiachia mikono yake kwa mara hiyo ilikuwa ni kama alikuwa anaachia kila kitu katika maisha yake macho yake yakaanza kudondosha machozi tena kama mtoto, na pendo pia alishindwa kujizuia , wote wakaanza kulia upya , waliangaliana na kila mmoja alitamani kumkumbatia mwenzake na kumueleza tafadhari usiondoke , lakini basi hilo lilipo waka injini na kuanza kurudi nyuma taratibu , ilikuwa ni ishara ya kwamba lazima pendo ashuke ndani ya basi hilo sekunde hiyo hiyo.
Alitembea huku bado macho yake yakimuamngalia wakati , ambae uso wake wote ulikuwa umelowa kwa machozi .
Alishuka na kwenda kusimama dirishani , waliangaliana huku wakitamani angalau kushikana mikono , lakini basi hilo lilikuwa refu kupita kiasi , waliinyoosha mikono yao lakini walishindwa kugusana hata vidole , japo pendo alirukia mkono huo.
Na gari liliendelea kurudi nyuma  na sasa lilianza kutoka nje ya stendi hiyo kweli na kuishika bara bara inayotoka nje ya mji wa lwangwa , pendo alikimbia kulifuata basi hilo kwa nyuma  nyuma.
“nitakusubiri mpenzi wangu, mimi na mwanetu tutakusubiri , najua utarejea, ninakwamini.”
Aliongea pendo kwa kupaza sauti.
“usijali mpenzi wangu , nakupenda sana , nakuahidi nitarejea.”
Wakati nae pia alipaza sauti , macho yao yalikuwa yakiangaliana , basi hilo lilitimua mbio na kuchanganya vumbi lililoipoteza picha  iliyokuwa kati yao , hakuna aliyekuwa anamuona mwenzake tena , bali vumbi zito lililomfanya kila mmoja akohoe na kuyafumba macho yake na hivyo ndivyo ilivyokuwa maono ya kila mmoja yalifunikwa na vumbi hilo na hivyo ndivyo walivyoagana, pendo alibaki amesimama akilia , huku wakati nae pia ndani ya basi akilia.
watu waliokuwa wakiwaangalia na waliwaona wa ajabu kweli.
***
Itaendelea kesho, pia unaweza kusoma stori sehemu ya mbele ya stori hii zaidi ya episodi 50 zipo tayari, pia unaweza kujipatia vitabu vyetu vingine kwa bei ya nafuu, kuna ofa ya vitabu kwa whatsap na inbox fb, viwili sh 1700 vitatu sh 2400
vinne sh 3200 vitano sh 4000,kimoja sh 1000.
Stori zetu zingine ni hizi zifuatazo:
NOT YOU NOW book 1 – 24 , MTOTO WA MTAA BOOK 1 – 20, I WILL HUNT YOU DOWN 1&2, WHEN I  SAY I LOVE 1 – 9, KIMBIA MPENZI BOOK 1,2,3,4,5 NA 6.  YOU CAN’T MAKE ME A FOOL AGAIN, SISTAHILI KUFUNGWA, NAIPENDA TANZANIA.
BABA WA KAMBO book01,
CHANGUO NGUO book01,02,03
TEKETEKE TAMU BOOK 01,02
YES BOSS BOOK 1,2, ASMA KIDOTI book 1,2,3 MSICHANA NYUMBA YA PILI BOOK1,2, KOCHA WA TENESI BOOK1,2, PITISHA KWENYE  MPASUO, WEZELE,
TWAMTOA MWARI book 1,2,
MCHEPUKO WA MSHUA, KITAA FLANI, MSAGAJI,
TAXI BUBU,
MAMA WA KAMBO BOOK 1,2,
DEMU WA GEREJI, MZEE WA CHUMVINI,
NATAKA ZOTE,
NIPE UTAMU KAKA JAMBAZI,
zamu zamu, OPARESHENI MAPENZI BOOK 1,2 JIRANI NYAMA YA HAMU BOOOK 1,2,3,4,5,6,7 NJOO MAMA HAYUPO 1,2,3,4,5,6 NATAKA UNIFUATE KICHAKANI BOOK 1,2,3,4,5 AISHA CHA UTAMU BOOK 1,2,3,4,5 KIDOLE AKINITOSHI BOOK 1,2,3  BEKI TATU WA MTAA BOOK 1,2,3,4
THE AFRICAN SEX MASHINE BOOK 1,2,3,4,5 na 6 KARIBU KITAA TICHA BOOK 
1,2,3,4,5 , KWAYA MASTA BOOK 1 , 2, 3 na 4 WIFI NIPE UTAMU … KAKA HAYUPO BOOK 1,2&3,4,5,6,7 , SHUGA MUMY LA 
KISTASHA BOOK 1,2,3. MUUZA MAZIWA BOOK 1- 16 , TOTO LA KISHUA 1- 9 , SI UNA MATE NIMEKUSIA BOOK 1 – 5,HALO HALO 1-9 JIMAMA MTAA WA PILI 1 -8
Namba zinazotumika kwa ajili ya malipo ni mpesa 0757 414 436 , tigo pesa 0715 557 191 airtel money 0789117674
Namba zote zimesajiliwa kwa jina la Deogratius Lwasye

No comments: