Tuesday 27 March 2018

KIMBIA MPENZI TUTAKUTANA MBELE KWA MBELE!! (Sehemu ya 11)


                                                    (the first run away love to told by Deogratius gift kipapa.)
EPISODI 11
INTRO:
Simulizi ya msichana wa shule aliyelazimika kumtorosha mpenzi wake mbali na baba yake pamoja na serikali mara baada ya kumpa ujauzito. Kamwe hakufikiri kwamba kumruhusu akimbie ni kuliruhusu penzi lake lipotelee mbali milele.  Simulizi hii, haitakuonyesha ni jinsi gani ilivyo kutengana na mpenzi wako pekee bali pia itakushangaza zaidi na uhusiano wa baba na mwana ambao kamwe hukuwahi kuuvutia picha, kuna machozi, na jasho, mbio na kuvuta pumzi, kama ulisoma simulizi yoyote ya mapenzi kutoka kwa gift kipapa na kuhakikishia ya kwamba haujasoma kitu. This is not just a heart to heart story but I run away love which no one could never ever found.
ILIPOISHIA EPISODI 10….
       “nakuja kwako , wakati , natuamaini tutakutana mpenzi wangu , na tutaishi maisha mazuri huko.”
Aliwaza pendo huku akitembea , kuelekea ilipo stendi ya mji huo, tayari ilikuwa imetimia mida ya saa kumi za alfajiri , na huo ulikuwa muda  muafaka kwa magari kuondoka kuelekea mji wa tukuyu.
Aliyakuta magari mawili na yote yalikuwa na abiria kadhaa , aliingia kwenye moja wapo na dakika kumi na tano baadae gari hilo lilianza kuondoka katika eneo hilo , na hiyo ilikuwa kwa heri ya pendo kwa mji wa itete na kwa wazazi wake pia.
MWENDELEZO WAKE:
Si kwamba ilikuwa mara yake ya kwanza kuingia katika jijiji la dare es salaam tu bali pia alikuwa hafamiani na mtu yoyote Yule anayeishi katika jiji hilo , aliposhuka ndani ya mabasi alibaki akishangaa tu, hakujua hata aanzie wapi , japo alikuwa anatembea kuufuata msululu wa abiria walioshuka pamoja nae kwenye basi, wakitoka rnje ya stendi hiyo ya ubongo.
“Tiketi iko wapi?”

Aliuliza mmoja kati ya watu waliokuwa wanatoza ushuru kwenye geti la kutokea nje ya stendi hiyo.
‘”hii hapa.”
Wakati alijibu mara baada ya kutoa tiketi yake kwenye mfuko wake wa suruali yake.”
Mtoza ushuru huyo alimruhusu kutoka mara baada ya kuridhika, aliendelea kuwauliza abiria wengine waliokuja nyuma yake.
Alikuwa nje sasa na kila kitu kilikuwa ni cha kushangaza zaidi , watu walikuwa wengi kupindukia , na wala hakukuwa na msululu kama ilivyokuwa mule ndani , kila mtu alishika njia yake na walijichanganya , huku madalali wa kukatisha tiketi wakikimbia huku na kule kugombaniana abiria waliokua anaingia ndani ya stendi hiyo.
Hapo wakati sasa alichanganyikiwa, alijaribu kusikiliza maongezi ya watu waliokuwa jirani yake wote walikuwa kama wanapiga kelele tu .
Mara huyu aliita taxi kwa abiria waliotoka , mwingine bajaji , mara aibuke dalali na kutangaza basi analolidalalia sehemu linapokwenda yani yani huku utasikia singida , mwingine Dodoma , iringa mbeya na huku wakitaja majina ya mabasi yao , kila kitu kwake kilikuwa kinamchanganya tu.
Hata angetaka kuchukua taxi au bajaji , isinge msaidia , kwani hadi wakati huo hajui hata aelekee wapi.
Akawa anatembea huku akishangaa jiji hilo, watu waliopita jirani yake walimpiga vikumbo, na kumfanya ayumbe huku na kule, aliiona njia iliyochepuka , akaifuata huku bado shingo yake ikigeuka kushangaa upande alipoyaona magorofa marefu.
“Oyaa!!”
Ilisika sauti hiyo na kumfanya Wakati ashtuke, aligeuka kumuangalia mtu huyo aliyekuwa anaongea  na hapo ndio akajikuta anashtuka zaidi , alikuwa ni mmoja kati ya wale vijana wa mjini waliozisokota nywele zao na kuchana chana suruali zao za jinsi , huku wakiwa wamezilegeza kwenye viuno vyao.
Macho yake yalikuwa mekundu na uso wake ulikuwa na makovu kadhaa, na vile sura yake alivyoikunja basi alizidi kumtisha Wakati.
“Naam.” aliitikia Kwa hofu huku akitetemeka.
“Lete begi hilo.”
Aliongea kwa ukali.
“Hizi ngu…o za..ngu.”
Aliongea kwa kigugumizi.
“lete pumbavu.”
Mwanaume huyo alisisitiza na kumfanya wakati azidi kutetemeka, wala hata hakujiuliza mara mbili, alimrushia begi hilo haraka.
“Mungu nisaidie.”
Alijisemesha kimoyo moyo.
“Hela zipo wapi?”
Aliuliza mvulana huyo kwa ukali.
“Kwenye soksi.”
Wakati alijikuta ameropoka, haukuwa mpango wake kumwambia alipozificha pesa zake lakini woga ndio uliomponza.
“lete hapa haraka.”
Alifoka tena, safari hii alitoa kisu kumuonyeshea, jambo lililomfanya wakati ajue kwamba huu sio mzaha.
Alivua viatu vyake haraka na kutoa pesa zake zote. Na kumkabidhi huku mwili wake ukizidi kutetemeka.
“Haya potea! Potea! haraka!”
Alipayuka kijana huyo na Wakati alikimbia bila hata ya kugeuka nyuma, akiwa ameshikilia viatu vyake mkononi.
Alikimbia mpaka akafika kwenye bara bara kubwa tena, alipogeuka nyuma, hakukuwa na yule kijana, alisimama na kuvaa viatu vyake.
Alitembea mpaka alipowakuta watu wengi wamesimama kwa pamoja kwenye kivuko cha bara bara wakisubiri magari yasimame ili wavuke.
Alisisimama pamoja nao , na magari yaliposimama akavuka pamoja nao.
Alitembea tu, lakini hadi muda huo, hakuongea na mtu yoyote wala kujua uelekeo wake , alikuwa akitembea tu  
***
Giza lilitanda huku bado akiendelea kutembea, jambo zuri ni kwamba hakuwa pekee yake katika bara bara hiyo , kulikuwa na watu wengine kibao ambao wao walikuwa na safari zao. Na hao ndio waliompa moyo wa kuwa huru kuzurura tu.
“Dar ndio hapa, sasa unaenda wapi?”
Alijiuliza baada ya kuchoshwa na safari isiyokuwa na muelekeo.
Akaamua kusimama na kuingiza mkono mfukoni, na kutoa saa yake isiyokuwa na mikanda, na kuiangalia.
“Saa sita!”
Alishtuka mara baada ya kuangalia kioo cha saa hiyo kupitia mwanga wa taa zilizokuwa zinamulika barabarani hapo.
“Natakiwa nitafute sehemu ya kupumzika.”
Aliwaza na kuanza kutembea tena, akitegemea kukutana na sehemu iliyojificha kidogo, kama kichochoro au kichaka ajipumzishe.
Alikuwa na bahati mara baada ya kuingia mmoja kati ya mitaa iliyokuwa na maduka yaliyofungwa , hapo alianza kuona watu walio lala nje ya maduka hayo wakiwa wametandika maboksi.
Jambo hilo lilimfanya atabasamu, alifurahi kuona idadi yote hiyo ya watu ambao  hawana sehemu ya kulala kama yeye.
Bila ya kuongea na yoyote alijisogeza sehemu iliyokuwa na uwazi na kujilaza, wala hata hakuitaji boksi au vipande vya magunia ambavyo aliviona sehemu walizolalia watu wengine , yeye alihitaji sehemu ya kulala tu.
Itaendelea kesho, pia unaweza kusoma stori sehemu ya mbele ya stori hii zaidi ya episodi 50 zipo tayari, pia unaweza kujipatia vitabu vyetu vingine kwa bei ya nafuu, kuna ofa ya vitabu kwa whatsap na inbox fb, viwili sh 1700 vitatu sh 2400
vinne sh 3200 vitano sh 4000,kimoja sh 1000.
Stori zetu zingine ni hizi zifuatazo:
NOT YOU NOW book 1 – 24 , MTOTO WA MTAA BOOK 1 – 20, I WILL HUNT YOU DOWN 1&2, WHEN I  SAY I LOVE 1 – 9, KIMBIA MPENZI BOOK 1,2,3,4,5 NA 6.  YOU CAN’T MAKE ME A FOOL AGAIN, SISTAHILI KUFUNGWA, NAIPENDA TANZANIA.
BABA WA KAMBO book01,02,03,
CHANGUO NGUO book01,02,03
TEKETEKE TAMU BOOK 01,02
YES BOSS BOOK 1,2, ASMA KIDOTI book 1,2,3 MSICHANA NYUMBA YA PILI BOOK1,2, KOCHA WA TENESI BOOK1,2, PITISHA KWENYE  MPASUO, WEZELE,
TWAMTOA MWARI book 1,2,
MCHEPUKO WA MSHUA, KITAA FLANI, MSAGAJI,
TAXI BUBU,
MAMA WA KAMBO BOOK 1,2,
DEMU WA GEREJI, MZEE WA CHUMVINI,
NATAKA ZOTE,
NIPE UTAMU KAKA JAMBAZI,
zamu zamu, OPARESHENI MAPENZI BOOK 1,2 JIRANI NYAMA YA HAMU BOOOK 1,2,3,4,5,6,7 NJOO MAMA HAYUPO 1,2,3,4,5,6 NATAKA UNIFUATE KICHAKANI BOOK 1,2,3,4,5 AISHA CHA UTAMU BOOK 1,2,3,4,5 KIDOLE AKINITOSHI BOOK 1,2,3  BEKI TATU WA MTAA BOOK 1,2,3,4
THE AFRICAN SEX MASHINE BOOK 1,2,3,4,5 na 6 KARIBU KITAA TICHA BOOK 
1,2,3,4,5 , KWAYA MASTA BOOK 1 , 2, 3 na 4 WIFI NIPE UTAMU … KAKA HAYUPO BOOK 1,2&3,4,5,6,7,  SHUGA MUMY LA 
KITASHA BOOK 1,2,3. MUUZA MAZIWA BOOK 1- 16, TOTO LA KISHUA 1- 9, SI UNA MATE NIMEKUSIA BOOK 1 – 5, HALO HALO 1-9, JIMAMA MTAA WA PILI 1 -8,
Namba zinazotumika kwa ajili ya malipo ni mpesa 0757 414 436 , tigo pesa 0715 557 191 airtel money 0789117674
Namba zote zimesajiliwa kwa jina la Deogratius Lwasye.

No comments: