Thursday 16 April 2015

WASIOJUA KUSOMA,KUANDIKA KUTOENDA DARASA LA TATU.


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Elimu), Kassim Majaliwa
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Elimu), Kassim Majaliwa

KATIKA kuhakikisha inaondoa kabisa tatizo la watu wasiojua kusoma na kuandika nchini, Serikali imefanya mabadiliko ambapo kuanzia sasa mtoto wa darasa la pili hawezi kuruhusiwa kuingia darasa la tatu kama hajui kusoma, kuandika na kuhesabu ili kuondoa tatizo la watoto wanaomaliza shule ya msingi wakiwa hawajui kusoma.
Pia imepunguza wingi wa masomo katika ngazi za chini kwa darasa la kwanza na la pili ambapo sasa watoto hao watasoma masomo matatu tu badala ya saba, huku ikifuta utaratibu wa walimu na watumishi wengine kulazimika kukubali vyeo kabla ya kuwarekebishia mishahara.
Kauli hiyo ilitolewa juzi na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) anayeshughulikia Elimu, Kassim Majaliwa wakati wa ufunguzi wa mafunzo kabilashi ya mtaala mpya kwa walimu wa darasa la kwanza na pili yanayofanyika katika ukumbi wa Chimwaga, Chuo Kikuu cha Dodoma.

No comments: