(the first run away love to told by Deogratius gift kipapa.)
EPISODI 06
INTRO:
Simulizi ya msichana wa shule aliyelazimika kumtorosha mpenzi wake mbali na baba yake pamoja na serikali mara baada ya kumpa ujauzito. Kamwe hakufikiri kwamba kumruhusu akimbie ni kuliruhusu penzi lake lipotelee mbali milele. Simulizi hii, haitakuonyesha ni jinsi gani ilivyo kutengana na mpenzi wako pekee bali pia itakushangaza zaidi na uhusiano wa baba na mwana ambao kamwe hukuwahi kuuvutia picha, kuna machozi, na jasho, mbio na kuvuta pumzi, kama ulisoma simulizi yoyote ya mapenzi kutoka kwa gift kipapa na kuhakikishia ya kwamba haujasoma kitu. This is not just a heart to heart story but I run away love which no one could never ever found.
ILIPOISHIA EPISODI 5….
“nitakusubiri mpenzi wangu, mimi na mwanetu tutakusubiri , najua utarejea, ninakwamini.”
Aliongea pendo kwa kupaza sauti.
“usijali mpenzi wangu , nakupenda sana , nakuahidi nitarejea.”
Wakati nae pia alipaza sauti , macho yao yalikuwa yakiangaliana , basi hilo lilitimua mbio na kuchanganya vumbi lililoipoteza picha iliyokuwa kati yao , hakuna aliyekuwa anamuona mwenzake tena , bali vumbi zito lililomfanya kila mmoja akohoe na kuyafumba macho yake na hivyo ndivyo ilivyokuwa maono ya kila mmoja yalifunikwa na vumbi hilo na hivyo ndivyo walivyoagana, pendo alibaki amesimama akilia , huku wakati nae pia ndani ya basi akilia.
watu waliokuwa wakiwaangalia na waliwaona wa ajabu kweli.
MWENDELEZO WAKE:
E6
Alishindwa kabisa kujizuia, kutengana na Wakati lilikuwa pigo kubwa sana kwake, machozi yaliendelea kumbubujika hata mbele ya mama yake , na kumganya mama yake ashtuke.
“pendo , unanini wewe?”
Aliuliza mama yake huku akishangaa.
Pendo alishindwa kumjibu lolote zaidi ya kumkabidhi barua aliyopewa shuleni.
“ya nini ?”
Aliuliza mama yake huku akiipokea , alianza kuifungua barua hiyo huku akimungalia pendo usoni, bado alikuwa analia.
“eti?”
Aliuliza mama yake kwa mshtuko mara baada ya kuifungua barua hiyo na kusoma haraka ili kupata kiini .
“Mungu wangu, we mtoto ni balaa gani hili ulilonitafutia!”
Aliuliza mama yake kwa mshituko huku pendio akiendeleza kilio cha kwikwi.
‘nani aliyekufanya hivi mwanangu?”
Aliuliza mama yake , na pendo aliendelea kulia tu bila kujibu lolote , jambo lililomfanya mama yake apatwe na hasira na kujikuta anamzaba kipao cha uso.
Hapo sasa kilio cha pendo kiliongezeka maumivu yote aliyokuwa anayapata moyoni sababu ya kutengana na mpenzi wake ndio kama vile yalifunguliwa na kibao hicho.
Mama yake alizidi kukasirika na kujikuta anampiga kibao kingine na kingine, pendo alizidi kulia kama vile mwenda wazimu.
“mwache , mwache mtoto , muache nimesema.”
Ilizikika sauti hiyo kwa ukali , alikuwa ni mzee Fanuel, baba yake pendo.
Mkoba wake aliuachia ukadondoka chini kisha haraka akaenda kumvuta binti yake toka kwa mkewe na kumkumbatia.
“nyamaza , nyamaza mama.”
Aliongea mr.fanuel huku akimbembeleza mwanae.
***
Alipofika mbeya mjini ilimbidi kulala ndani ya basi ili kuisubiri safari itakayofanyika alfajiri ya siku inayofuta basi hilo lililoandikwa KILIMANJARO ubavuni mwake lilikuwa na watu wengine wasiopungua ishirini ambao nao pia walitarajia kufanya safari aflajiri hiyo.
E11 ndio kiti ambacho wakati alikuwa amekalia, kililikuwa ni kiti cha dirishani , alichagua kiti hicho ili awe anaona mazingira basi likiwa safarini.
“mama, mama ,mbona basi aliendi?”
Aliomngea mtoto mmoja aliyekuwa amekaa na mma yake kicha pembeni ya wakati .
“litaenda tu mwanangu subiri kwanza tukiamka.”
Aliongea mama wa mtoto huyo.
“nilale?”
Aliuliza mtoto huyo.
“ndio lala mwanangu.”
Alimjibu mama yake.
“sawa kitanda kiko wapi?”
Aliuliza.
“lala hivyo hivyo bwana mi nimechoka .”
Aliongea mama huyo kwa ukali , sauti hiyo ilimtisha mwanae na kumfanya aanze kulia , kichwani mwake alifikiri mama yake atampiga muda huo huo.
“basi baba basi , nyamaza mwanangu.”
Aliongea mama huyo huku akimbembeleza mwanae mpaka akatulia. Wakati aliwaangalia kisha akaamuakugeukia upande wa dirishani , ambapo alijikuta amechukuliwa na usingi8zi dakika chache tu baada ya kufumba macho.
***
Itaendelea kesho, pia unaweza kusoma stori sehemu ya mbele ya stori hii zaidi ya episodi 50 zipo tayari, pia unaweza kujipatia vitabu vyetu vingine kwa bei ya nafuu, kuna ofa ya vitabu kwa whatsap na inbox fb, viwili sh 1700 vitatu sh 2400
vinne sh 3200 vitano sh 4000,kimoja sh 1000.
Stori zetu zingine ni hizi zifuatazo:
NOT YOU NOW book 1 – 24 , MTOTO WA MTAA BOOK 1 – 20, I WILL HUNT YOU DOWN 1&2, WHEN I SAY I LOVE 1 – 9, KIMBIA MPENZI BOOK 1,2,3,4,5 NA 6. YOU CAN’T MAKE ME A FOOL AGAIN, SISTAHILI KUFUNGWA, NAIPENDA TANZANIA.
BABA WA KAMBO book01,
CHANGUO NGUO book01,02,03
TEKETEKE TAMU BOOK 01,02
YES BOSS BOOK 1,2, ASMA KIDOTI book 1,2,3 MSICHANA NYUMBA YA PILI BOOK1,2, KOCHA WA TENESI BOOK1,2, PITISHA KWENYE MPASUO, WEZELE,
TWAMTOA MWARI book 1,2,
MCHEPUKO WA MSHUA, KITAA FLANI, MSAGAJI,
TAXI BUBU,
MAMA WA KAMBO BOOK 1,2,
DEMU WA GEREJI, MZEE WA CHUMVINI,
NATAKA ZOTE,
NIPE UTAMU KAKA JAMBAZI,
zamu zamu, OPARESHENI MAPENZI BOOK 1,2 JIRANI NYAMA YA HAMU BOOOK 1,2,3,4,5,6,7 NJOO MAMA HAYUPO 1,2,3,4,5,6 NATAKA UNIFUATE KICHAKANI BOOK 1,2,3,4,5 AISHA CHA UTAMU BOOK 1,2,3,4,5 KIDOLE AKINITOSHI BOOK 1,2,3 BEKI TATU WA MTAA BOOK 1,2,3,4
THE AFRICAN SEX MASHINE BOOK 1,2,3,4,5 na 6 KARIBU KITAA TICHA BOOK
1,2,3,4,5 , KWAYA MASTA BOOK 1 , 2, 3 na 4 WIFI NIPE UTAMU … KAKA HAYUPO BOOK 1,2&3,4,5,6,7 , SHUGA MUMY LA
KISTASHA BOOK 1,2,3. MUUZA MAZIWA BOOK 1- 16 , TOTO LA KISHUA 1- 9 , SI UNA MATE NIMEKUSIA BOOK 1 – 5,HALO HALO 1-9 JIMAMA MTAA WA PILI 1 -8
Namba zinazotumika kwa ajili ya malipo ni mpesa 0757 414 436 , tigo pesa 0715 557 191 airtel money 0789117674
Namba zote zimesajiliwa kwa jina la Deogratius Lwasye
Thursday, 15 March 2018
KIMBIA MPENZI TUTAKUTANA MBELE KWA MBELE!!(Sehemu ya 6)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment