MICHEZO


 

 

 

Chelsea waongoza kwa utovu wa nidhamu England

27A8D17200000578-3043181-image-a-16_1429259580822
Takwimu zilizotolewa na maafisa wa mchezo wa kiungwana wa FA zinaeleza kuwa Chelsea ni timu inayoongoza kutoheshimu maamuzi ya waamuzi katika ligi kuu England, huku makocha wa timu hiyo wakishika nafasi ya pili kwa utovu wa nidhamu wakati wa mechi.

Liverpool imetajwa kuwa klabu yenye heshimu kubwa kwa waamuzi katika kipengele hicho kilichobeba alama saba ikifuatiwa na Burnley na West Brom.

Klabu za Arsenal na Stoke City zipo katikati katika orodha hiyo ambapo kanuni zinaeleza kuwa kitendo cha kuheshimu maamuzi yenye utata bila kugoma au kumzonga muamuzi kinaipa timu alama saba wakati tabia ya kukubali maamuzi halafu kuonesha ishara za kutoheshimu zinatolewa alama sita.(P.T)

FA wanatoa alama kwa kuangalia maeneo sita ambayo ni kadi nyekundu na njano, mchezo mzuri, heshima kwa wapinzani, heshima kwa waamuzi, tabia ya maafisa wa timu na mashabiki.

Alama kumi zinatolewa kwa kadi nyekundu ambapo timu inapunguziwa alama moja kwa kadi ya njano na alama tatu kwa kadi nyekundu.

Mchezo mzuri una alama kumi zinazotolewa kwa kucheza soka la kuvutia, kushambulia sana na kushinda, lakini timu ikitumia mbinu za kujilinda na udanganyifu alama zinapunguzwa.

Alama saba zinatolewa katika kipengele cha heshima kwa wapinzani kinachohusisha kuwaheshimu wachezaji pinzani na kuonesha mchezo wa kiungwana, wakati alama saba pia zinatolewa kwa kuheshimu waamuzi na maafisa wa mechi.

Alama sita zinatolewa kwa maafisa wa timu wakiwemo makocha dhidi ya waamuzi, wakati alama kumi zinatolewa kwa tabia ya mashabiki ambapo alama zote zinatolewa kwa mashabiki wanaokubali matokeo, wakati wakitumia lugha ya matusi kwa wachezaji, waamuzi na kuwatishia mashabiki pinzani alama zinapounguzwa.

 

 


Luis Suarez amefunga mabao mawili wakati Barcelona ikiichapa PSG kwa mabao 3-1.

Bao la kwanza lilifungwa na Neymar, Suarez akafunga la pili ambalo likawa la 1,000 kabla ya kufunga tena ambalo limekuwa bao la 1,001.

Pamoja na kufikisha mabao hayo, Barcelona inaendelea kubaki katika nafasi ya pili kwa kuwa Real Madrid ndiyo inayoongoza kwa kuwa na mabao 1,016.

WENYE MABAO MENGI ULAYA
Real Madrid  1,016
Barcelona      1,001
Bayern            823
Juventus         748


Bayern yaangukia pua,Barcelona kidedea






mambo ya viwanjani kila mmoja kwa namna ya ushangiliaji wake wa goli.

Mechi za klabu bingwa barani Ulaya katika hatua ya robo fainali ziliendelea tena usiku wa kuamkia leo kwa michezo miwili kupigwa. Bayern Munich walikuwa ugenini kukipiga na FC Porto ya Ureno. Katika hali isiyotarajiwa na wengi Bayern imeangukia pua kwa kucharazwa mabao 3-1.
Nako nchini Ufaransa wenyeji Paris Saint German ilishuka dimbani kuikabili miamba ya soka ya Hispania Barcelona. Katika mchezo huo wenyeji PSG wamejiweka katika hali ngumu baada ya kucharazwa mabao 3-1. Bao la Neymar jr na mawili ya Luis Suárez yalitosha kuwazamisha wenyeji wao na kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele.
Timu zote nne zitacheza michezo ya marudiano April 21 siku ya Jumanne.

KIKOSI CHA BARCELONA KIMEENDELEA NA MAZOEZI VIZURI HUKU WACHEZAJI WAKE WAKIONEKANA WAKO TAYARI KUIVAA PSG KESHO KATIKA MECHI YAO YA KWANZA YA ROBO FAINALI YA LIGI YA MABINGWA ULAYA WAKIWA UGENINI. WACHEKI MWENYEWE....







14Apr2015

Beki wa Real Madrid, Marcelo amewataka mashabiki wa timu hiyo kuondoa hofu kuhusiana na mchezo wa leo usiku.


Real Madrid itakuwa ugenini katika mchezo wake wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya wapinzani wao wakubwa Atletico Madrid.

Marcelona amewaambia mashabiki wao kuwa licha ya kuonekana wanasumbuliwa sana na wapinzani wao hao, wao wanajua watakachokifanya.

“Itakuwa kazi ngumu, lakini tunajua tutakachokifanya. Watuamini,” alisema.


Mechi hiyo inasubiriwa kwa hamu kwa kuwa Real Madrid ndiyo mabingwa, mashabiki wanaingia hofu ya kupoteza ubingwa huo.

No comments: