Friday 14 June 2013

WANAHABARI 13 KATI YA 18 WASHINDA TUZO ZA TANAPA 2012 TANAPA MEDIA AWARDS






 Uharibifu  wa vyanzo  vya maji katika kingo  za mto  Ruaha unaomwaga maji yake katika  hifadhi ya Taifa  ya Ruaha umeendelea  kuwatesa  wanyama  ambao maisha uhai  wao  wanategemea maji  zaidi kama anavyoonekana mnyama huyu aina ya boko akihangaika  kuchimba maji ardhini kwa miguu leo ,kama alivyonaswa na kamera ya matukio  daima  iliyopo hifadhini hapo

...................................................................................................................................................
 
WAZIRI wa maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki amekabidhi kwa mara ya kwanza tuzo umahili wa uandishi wa habari za uhifadhi zilizoandaliwa na shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA ) SHIRIKA la hifadhi ya Taifa (TANAPA ) 2012 TANAPA MEDIS AWARDS 
 
Akikabidhi tuzo hizo usiku wa kuamkia leo  katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Wiloles HIlltop mjini Iringa waziri Kagasheki alisema kuwa anasikitishwa na idadi ndogo ya washiriki katika shindano hilo na kuwa baadhi ya tuzo zimebaki kwa kukosa washiriki hivyo kuwataka wanahabari nchini kuchangamkia kuingika katika shindano hilo.
 
Waziri Kagasheki alisema kuwa lengo la TANAPA kuanzisha tuzo hizo kwa wanahabari ni kutaka kuona wanahabari wanaandika kwa usahihi na ubora mkubwa habari za uhifadhi ikiwa ni pamoja na kufichua vitendo vya ujangili katika hifadhi hizo .
 
Hivyo aliwataka wanahabari ambao wameshinda tuzo hizo na wale ambao hawakushinda kuendelea kuandika habari za uhifadhi na pale wanapatakiwa kushiriki katika shindano kujitokeza kushindanisha kazi zao.
 
"Shabaha ya wizara kuanzisha tuzo hizi ni kuwapa moyo wa kuendelea kuifanya kazi hiyo kwa ubora ikiwa ni pamoja na kufanya tafiti mbali mbali"
 
Hivyo kuwataka TANAPA kuendelea kuboresha zaidi tuzo hiyo kama njia ya kuwawezesha wanahabari wengi zaidi kujitokeza ili mwisho wa siku kuweza kuieleza dunia juu ya uhifadhi unaofanywa na Taifa katika uhifadhi.
 
Kwani alisema kuwa wizara yake inawategemea zaidi wanahabari na vyombo vya habari katika kupambana na vitendo vya ujangili.
 
Waziri Kagasheki alisema kuwa mkakati wa wizara yake ni kuitisha mkutano mkubwa wa wadau wa utalii utakaofanyika mwezi Novemba mwaka huu kwa ajili ya kutafuta njia sahihi ya kudumu katika kutokomeza ujangili wa wanyama katika hifadhi hapa nchini .
 
Alisema kuwa tatizo la kuuwawa kwa Tembo duniani ni kubwa katika nchi ya Botswana na Tanzania ni ya pili hivyo haitapendeza mikutano mikubwa ya kupambana na ujangili kufanyika nchi za ulaya ambazo hakuna tatizo hilo badala ya nchi husika kama Tanzania.
 
Pia alisema kuwa mbali ya wizara yake kuanzisha utaratibu huo wa kuwapongeza wanahabari wanaosaidia katika kuhamasisha uhifadhi na kufichua vitendo vya ujangili bado anapongeza jitihada kubwa zinazofanywa na vyombo vya habari nchini katika kukemea vitendo vya ujangili nchini .
 
Awali Ofisa Uhusiano wa Tanapa Paschal Shelutete alisema kuwa awali tuzo hizo zilikuwa zikitolewa na baraza la habari Tanzania (MCT) ila kutokana na tathimini waliyoifanya wao wakaona ni vema tuzo hizo kuzitoa katika orodha ya tuzo za MCT na kuzifanya wenyewe TANAPA .
 
Kwani alisema kuwa lengo la TANAPA ni kuona habari zinazoandikwa zinakuwa na ubora wa hali ya juu na zinaendana na malengo ya Taifa katika uhifadhi hivyo katika mwaka huu ambao ni mwaka wa kwanza kuzitoa zoezi la kuwapata washindi wa tuzo hizo lilisimamiwa na jaji mkuu Dr Ayub Rioba pamoja na majaji wengine ambao wamebobea katika tasnia ya habari na masuala ya hifadhi .

Aliwataja walioshinda upande wa magazeti kundi la uhifadhi ni Albano Midelo NIpashe /Kiongozi aliyezawadiwa cheti ,hundi ya Tsh milioni 1.5 ,ngao na safari ya siku saba katika nchi za kusini mwa Afrika kwa kujifunza masuala ya hifadhi Mussa Juma (Mwananchi) aliyeibuka mshindi wa pili alipata cheti,hundi ya Tsh milioni 1 na watatu ni David Azaria -Habari alizawadiwa cheti na hundi ya Tsh.500,000

Wakati mshindi wa kwanza katika kundi la Radio ambaye hata hivyo alikuwa mmoja ni
Mshindi wa kwanza upande wa Radio ni Alex Magwiza -TBC aliyezawadiwa cheti ,ngao ,hundi ya Tsh milioni 1.5 na safari ya siku saba katika nchi za kusini mwa Afrika .
 
Wakati kundi TV upande wa uhifadhi alikuwa mshindi mmoja pekee Festo Sikaganamo (ITV) aliyeshinda ngao,hundi ya Tsh milioni 1.5 na safari ya kujifunza utalii nchi za kusini mwa Afrika.
 
Wakati tuzo ya utalii wa ndani upande wa magazeti mshindi wa tatu ni Elia Mbonea (RAI)cheti na hundi ya Tsh 500,000 wakati mshindi wa pili ni Salome Kitomari (Nipashe) aliyepata cheti na hundi ya Tsh milioni 1 wakati mshindi wa kwanza alikuwa Phinias Bashaya -Mwananchi aliyeshinda ngao,hundi ya Tsh milioni 1.5 na safari ya kujifunza utalii nchi za kusini mwa Afrika.
 
Eneo la utalii wa ndani vipindi vya radio wa kwanza ni ni Alex Magweza (TBC) aliyeshinda ngao,hundi ya Tsh milioni 1.5 na safari ya kujifunza utalii nchi za kusini mwa Afrika na wa pili David Rwenyagira (Radio One) aliyepata cheti na hundi ya Tsh milioni 1

Upande wa utalii wa ndani katika TV ni Juma Nugaz ( Clouds Tv) cheti na hundi ya Tsh 500,000 aliyeshika nafasi ya tatu ,mshindi wa pili ni Raymond Nyamwihula (Star TV) wakati mshindi wa kwanza ni Lilian Shirima (TBC)

No comments: