Sunday, 11 March 2018

KIMBIA MPENZI TUTAKUTANA MBELE KWA MBELE!! (Sehemu ya pili)


                                                    (the first run away love to told by Deogratius gift kipapa.)
EPISODI 02
INTRO:
Simulizi ya msichana wa shule aliyelazimika kumtorosha mpenzi wake mbali na baba yake pamoja na serikali mara baada ya kumpa ujauzito. Kamwe hakufikiri kwamba kumruhusu akimbie ni kuliruhusu penzi lake lipotelee mbali milele.  Simulizi hii, haitakuonyesha ni jinsi gani ilivyo kutengana na mpenzi wako pekee bali pia itakushangaza zaidi na uhusiano wa baba na mwana ambao kamwe hukuwahi kuuvutia picha, kuna machozi, na jasho, mbio na kuvuta pumzi, kama ulisoma simulizi yoyote ya mapenzi kutoka kwa gift kipapa na kuhakikishia ya kwamba haujasoma kitu. This is not just a heart to heart story but I run away love which no one could never ever found.
ILIPOISHIA EPISODI 01….
“Ni mgeni ndio , baba yangu ameamishiwa hapa kikazi.”
Aliongea pendo.
‘ni daktari?”
Aliuliza
“ndio , kwa nini?”

 “nafikiri nina mjua , niliongea na daktari mpya wiki mbili zilizopita , alinitaka nimpelekee kiti moto nyumbani kwake.”
 Aliongea wakati.
“ni kitu gani kimekufanya ufikiri ni baba yangu?”
Aliuliza .
“namjua kila mtabibu anayefanya kazi katika hospitali ya itete , huu ni mji mdogo pendo.”
Aliongea wakati huku akitabasamu.

MWENDELEZO WAKE:
Na kisha akasogea mahali sehemu anayopimia na kuwapimia wateja kadhaa , kutia ndani yule msichana aliyekuwa anataka kachumbari , na kisha kurudi kwa pendo aliichukua oda yake pia nakumpimia, lakini hakumuacha ale kwa amani , muda wote alikuwa pembeni yake akijaribu kuongea chochote , japo wateja zaidi waliongezeka na kumfanya anyanyuke mara kadhaa kuwahudumia, lakini siku hiyo ilikuwa mwanzo wa safari yao ya mapenzi na kila mmoja alijua.
Na katika hali ambayo hakuna yoyote kati yao aliyeitegemea wakajikuta katika penzi zito lililoichota mioyo yao na kumfanya kila mtu ashindwe kuitambua nafsi yake tena, ni kama vile kila mmoja alikuwa ameutoa moyo wake na kuukabidhi kwa mwenzie.

Kila mtu alikuwa na furaha mno na walikuwa wanataka maisha yao yote yawe hivyo, walikuwa na ndoto ya pamoja , pendo kusoma kwa bidiii zake zote mpaka kuwa daktari katika hospitali ya itete kama baba yake  na upande wa  wakati ilikuwa kufanya bidii katika kazi yake mpaka afanikishe ndoto yake ya kujenga hoteli ya kwanza yenye hadhi ya juu katika mji huo. Ndoto zao zilikuwa safi na zilimfanya kila mtu apate chachu katika kile anachokifanya kupita kiasi.
Pendo alifanikiwa kushika namba moja katika masomo yake yote ya sanyansi huku wakati akifanikisha kukusanya pesa hadi alisimia themanini ya kipato chake chote alichokipata alilazimika kuiweka akiba, na kwa kweli alikuwa anaenda vizuri , lakini huu ugonjwa wa bibi yake pamoja na kifo chake kilichukuwa kila kitu alichokuwa nacho, matumizi pamoja na gharama za hospitali vilimaliza akiba yake yote , huku msiba ukimaliza nguvu kazi yake yote.
Na sasa baada ya kila kitu kupita , wakati hakuwa na lolote la kufanya zaidi ya kutulia chini na kuanza tena mapambano, ili kuunyanyua tena mnara wa ndoto yake pamoja na mpenzi wake.
Alifanya usafi katika kibanda chake na kuanza kuosha vyombo ambavyo anatakiwa kufanyia biashara.
Sufuria bakuri na kila kitu.
Akiwa katikati ya shughuli hiyo ndipo alipomuona pendo na sare za shule  akija huku analia, kwa kweli hili halikuwa jambo la kawaida , wakati alishtuka sana na kuacha kila kitu na kumkimbilia haraka. Alishasahau kwamba hawakupaswa kufanya hivyo mbele ya watu, kila siku pendo alikuwa akija hapo kama mteja , lakini leo vibanda vyote vya jirani viliona jinsi wakati anavyomhangaikia pendo.
Waliingia kibandani na pendo badala ya kusema chochote aliendelea kulia.
Jambo lililomfanya wakati achanganyikiwe.
Unatatizo gani mpenzi! Tafadhari niambie unanifanya nilie bila hata ya kujua sababu.”
Aliongea wakati huku machozi yakimlenga kwa kweli , alishindwa kujizuia , kumuangalia pendo akilia peke yake wakati wote.
“nina mimba , Wakati!”
Aliongea pendo neno ambalo lilimaliza nguvu zote za wakati, kwa kweli alitarajia lolote kutoka kwake lakini sio jambo hilo.
“umejuaje hilo , labda una wasi wasi tu? pendo tafadhari niambie huna uhakika na hilo.”
Aliongea wakati huku akilia.
Lakini pendo hakujibu lolote zaidi ya kumpa wakati bahasha.
“ya nini?”
Aliuliza wakati huku akishangaa.
“imetoka shule , tayari nimefukuzwa shule, wametupima na wametufukuza wote tuliokuwa na mimba.”
Aliongea pendo huku akiendelea kulia. Wakati ndio alizidi kuwa hoi, hii kwakwe ilikuwa kama vile ndoto ya kutisha.
“tutafanya nini pendo, vipi kuhusu ndoto zetu , tutafanya nini mpenzi wangu, watanikamata na kunifunga miaka thelathini , nitakwenda kufa huko na nitakupoteza daima , siko tayari kukupoteza pendo , wewe ndio mtu pekee niliyobakia nae katika maisha, sitaki kukupoteza.”
Aliongea wakati huku akiwa amechanganyikiwa, mashavu yake yote yaliokuwa yamelowa machozi na alikuwa mwenye wasi wasi mkubwa.
“hapana , hautonipoteza , wakati, hakuna atakaye kufunga na wala hatutapoteza ndoto yetu hata moja, utakuwa unamiliki mgahawa wenye hadhi ya juu itete nzima na mimi nitakuwa daktari bingwa,umenisikia,  umenisikia mimi?”
Aliongea pendo akiwa amemshika bega wakati , ambaye alikuwa akitetemeka wakati wote , kwa kweli akuwa na wasi wasi mkubwa juu ya kila kitu.
“hilo litawezekana vipi pendo , wamesha kufukuza shule tayari , na wakati wowote askari watatumwa kuja kunisaka , yote haya yamekwisha pendo , yamekwisha , kila kitu kinakufa baada ya bibi kufa , labda kwa sababu yeye ndio mtu pekee aliyekuwa anajua siri ya penzi letu , hivyo kwa kuwa amekufa basi kila kitu kina kuwa wazi , ninaogopa sana pendo , unamjua baba yako, hawezi kuniacha, amekuwa akiwa piga watu ambao wanakuongelesha tu njiani je vipi kuhusu mimi niliye kupa mimba kabisa?”
Aliongea wakati huku akilia.
Itaendelea kesho, pia unaweza kusoma stori sehemu ya mbele ya stori hii zaidi ya vitabu 6 vipo hewani sasa, pia unaweza kujipatia vitabu vyetu vingine kwa bei ya nafuu, kuna ofa ya vitabu kwa whatsap na inbox fb, viwili sh 1700 vitatu sh 2400
vinne sh 3200 vitano sh 4000,kimoja sh 1000.
Stori zetu zingine ni hizi zifuatazo:
 NOT YOU NOW book 1 – 24 , MTOTO WA MTAA BOOK 1 – 20, I WILL HUNT YOU DOWN 1&2, WHEN I  SAY I LOVE 1 – 9, KIMBIA MPENZI BOOK 1,2,3,4,5 NA 6.  YOU CAN’T MAKE ME A FOOL AGAIN, SISTAHILI KUFUNGWA, NAIPENDA TANZANIA.
BABA WA KAMBO book01,
CHANGUO NGUO book01,02,03
TEKETEKE TAMU BOOK 01,02
YES BOSS BOOK 1,2, ASMA KIDOTI book 1,2,3 MSICHANA NYUMBA YA PILI BOOK1,2, KOCHA WA TENESI BOOK1,2, PITISHA KWENYE  MPASUO, WEZELE,
TWAMTOA MWARI book 1,2,
MCHEPUKO WA MSHUA, KITAA FLANI, MSAGAJI,
TAXI BUBU,
MAMA WA KAMBO BOOK 1,2,
DEMU WA GEREJI, MZEE WA CHUMVINI,
NATAKA ZOTE,
NIPE UTAMU KAKA JAMBAZI,
zamu zamu, OPARESHENI MAPENZI BOOK 1,2 JIRANI NYAMA YA HAMU BOOOK 1,2,3,4,5,6,7 NJOO MAMA HAYUPO 1,2,3,4,5,6 NATAKA UNIFUATE KICHAKANI BOOK 1,2,3,4,5 AISHA CHA UTAMU BOOK 1,2,3,4,5 KIDOLE AKINITOSHI BOOK 1,2,3  BEKI TATU WA MTAA BOOK 1,2,3,4
THE AFRICAN SEX MASHINE BOOK 1,2,3,4,5 na 6 KARIBU KITAA TICHA BOOK
1,2,3,4,5 , KWAYA MASTA BOOK 1 , 2, 3 na 4 WIFI NIPE UTAMU … KAKA HAYUPO BOOK 1,2&3,4,5,6,7 , SHUGA MUMY LA
KISTASHA BOOK 1,2,3. MUUZA MAZIWA BOOK 1- 16 , TOTO LA KISHUA 1- 9 , SI UNA MATE NIMEKUSIA BOOK 1 – 5,HALO HALO 1-9 JIMAMA MTAA WA PILI 1 -8
Namba zinazotumika kwa ajili ya malipo ni mpesa 0757 414 436 , tigo pesa 0715 557 191 airtel money 0789117674
 Namba zote zimesajiliwa kwa jina la Deogratius Lwasye

No comments: