Mbunge
wa Iringa Mjini(Chadema), Mchungaji Peter Msigwa amesema atalishitaki
Jeshi la Polisi, kwa tuhuma za kuingilia majukumu yake ya kikazi pale
anapokuwa akitimiza wajibu wake wa kibunge ikiwemo kuongea na wananchi.
Mchungaji
Msigwa amesema atakata rufaa kwa sababu polisi wamezuia mikutano yake
ya leo na kesho ambayo alitarajia kufanya katika kata za Kihesa na
Kitwiru kwa madai ya kukiuka masharti alipohutubia katika Kata ya
Mlandege.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Jumatatu, Mchungaji Msigwa amesema chombo
pekee kinachoweza kumtia hatiani kwa kufanya uchochezi ni Mahakama na
sio polisi.
“Jana
walinikamata tangu saa 11:30 na kuanza kunihoji mpaka saa 3:15 usiku
kwa tuhuma za kufanya uchochezi lakini mimi nakataa sijafanya uchochezi
kwa sababau hakuna mtu anaweza kunizuia kuongea na wananchi wangu,
wanadai nimeleta hofu na kuvichonganisha vyombo vya dola na wananchi,”
amesema Mchungaji Msigwa .
Amesema
mpaka muda huu yupo nje kwa dhamana na tayari ameripoti polisi asubuhi
leo Jumatatu amehojiwa lakini ameambiwa ataitwa tena kwa mahojiano
zaidi.
“Mimi
niko tayari hata kama wangeniweka ndani wiki mbili siogopi kwa sababu
sitanyamaza nitaendelea kuongea na sitaacha kusema kilichomtokea Tundu
Lissu na ili kuninyamazisha ni lazima waniue kwa sababu nishajiandaa
kisaikolojia,” amesema Mchungaji Msingwa.
Akizungumzia
hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Julius Mjengi amesema
walimkamata Msigwa kwa kuwa alikuwa anatoa maneno ya uchochezi kwa
wananchi aliokuwa anawahutubia mkutano wa hadhara Kata ya Mlandege.
Mgengi
amesema bado jeshi hilo linaendela na upelelezi juu ya tuhuma hizo na
mara utakapokamilika watamfikisha mahakamani mbunge Msigwa.
No comments:
Post a Comment