Tunaitakia kila la kheri timu ya Tanzania katika mchezo huo muhimu , tunaamini maandalizi yametimia na kikosi kipo tayari kwa mchezo huu muhimu na tuna imani kubwa kuanzia na benchi la ufundi na wachezaji wote kwa ujumla.
Kufanya vizuri kwa timu ya taifa ni mwanzo mpya wa taifa letu hasa katika kipindi hiki cha mchakato wa katiba mpya , Michezo uondoa tofauti zetu za kisiasa , kikabila nk hivyo kufanikiwa kupata ticket ya kwenda Brazil itatuunganisha watanzania katika kipindi hiki cha maandalizi ya kupata katiba mpya.
Mungu ibariki Taifa Stars ,Mungu ibariki Tanzania
No comments:
Post a Comment