Friday, 7 June 2013

UINGEREZA KUWALIPA MAUMAU


Serikali ya Uingereza kwa mara ya kwanza imetambua mateso na ukandamizaji vilivyofanywa na maafisa wake wa kikoloni katika operesheni za kuzima uasi wa Mau Mau nchini Kenya mnamo miaka ya 1950. 
 Some of the four Kenyans who are taking The British government to court, with left-right; Wambugu Wa Nyingi, Jane Muthoni Mara, Paulo Nzili, outside the Royal Courts of Justice, in central London, Thursday, April 7, 2011, as four elderly Kenyans who claim that they were severely beaten and tortured by British officers during an anti-colonial rebellion in the 1950s are taking their case to court in London. The Kenyans, claiming to be victims of British colonial era torture during the 'Mau Mau' rebellion by Kenyans against British rule, are giving evidence of their claims against the British Government. (ddp images/AP Photo/Lefteris Pitarakis)
Hata hivyo nchi hiyo imesema haiwajibiki kutokana na vitendo hivyo vilivyofanywa na watawala wa kikoloni, na badala yake imekubali kulipa fidia ya kiasi cha euro milioni 23 kwa wazee takribani 5000 nchini Kenya ambao waliathiriwa na vitendo hivyo. Kila mmoja wa wazee hao atapata kiasi cha Euro 4,700. 
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uingereza William Hague aliomba radhi kwa niaba ya serikali yake, kwa kile alichokiita uvunjaji wa haki za binadamu uliovuruga mchakato wa kupigania uhuru wa Kenya. Alisema Uingereza inavilaani vitendo hivyo kwa nguvu zote.

No comments: