Saturday 10 March 2018

HADITHI YA KIMBIA MPENZI TUTAKUTANA MBELE KWA MBELE!!

KIMBIA MPENZI TUTAKUTANA MBELE KWA MBELE!!
                                                    (the first run away love to told by gift kipapa.)
EPISODI 01
INTRO:
Simulizi ya msichana wa shule aliyelazimika kumtorosha mpenzi wake mbali na baba yake pamoja na serikali mara baada ya kumpa ujauzito. Kamwe hakufikiri kwamba kumruhusu akimbie ni kuliruhusu penzi lake lipotelee mbali milele.  Simulizi hii, haitakuonyesha ni jinsi gani ilivyo kutengana na mpenzi wako pekee bali pia itakushangaza zaidi na uhusiano wa baba na mwana ambao kamwe hukuwahi kuuvutia picha, kuna machozi, na jasho, mbio na kuvuta pumzi, kama ulisoma simulizi yoyote ya mapenzi kutoka kwa gift kipapa na kuhakikishia ya kwamba haujasoma kitu. This is not just a heart to heart story but I run away love which no one could never ever found.
MWANZO WA STORI:
Lilikuwa pigo kubwa sana baada ya bibi yake mpendwa kupoteza maisha , alikuwa ndio ndugu pekee aliyekuwa nae , katika ulimwengu huu , kijana huyu alilia kupita kiasi , aliposhuhudia jinsi wanaume hawa wa kijiji wakiushusha mwili wa bibi yake uliokuwa umezungushwa kwenye mikeka , huku wanawake wa kwaya ya umoja wa kinamama wakiimbia wimbo wa kumuaga , Wakati alishindwa kujizuia kabisa , alishikwa huku na huku na wanaume waliokuwa jirani yake , lakini bado alikuwa akifurukuta akilia na kusogelea kabuli ili nae aingie kwenye shimo la kabuli, na kama kufukiwa basi afukiwe pamoja nae.
Kilikuwa kilio kwa watu wote walikuwepo makaburini hapo, kwa kweli walimuonea huruma sana Wakati, kuishi kwenye jamii bila ndugu yoyote yule lilikuwa jambo la kusikitisha sana. Na tena ukizingatia umri wake , bado alikuwa mvulana tu, aliyekuhitaji kuangaliwa na mtu fulani.
Wiki nzima msiba huo bado ulikuwa unaendelea kwa wakati, alikuwa anajifungia ndani ya kibanda chake na kulia pekee yake , kulikuwa na mtu mmoja tu ambae alikuwa anafika hapo kumuona mara baada ya msiba.

Na ni yeye ndio aliyekuwa akimjali kwa kila kitu, chakula, mavazi  na hata kumfariji wakati wote , alidiriki hata kusimamisha masomo yake kwa wiki hiyo yote bila ya wazazi wake kujua. Huyu msichana mrembo kuliko msichana yoyote yule katika mji wa itete , alikuwa ndio mtu pekee aliyebaki nae.
Alimpenda msichana huyu na yeye alimpenda pia , penzi lao lililokuwa likiendeshwa kwa siri kubwa ndio lilikuwa penzi lenye nguvu kuliko penzi la uhusiano wowote katika mji huo.
“nakushukuru sana pendo , unanifanya nisijisikie pekee yangu tena, wewe ni mpenzi bora zaidi daima.”
Aliongea wakati akiwa amekumbatiana na pendo wakiwa juu ya kitanda chake alichokitengeneza mwenyewe kwa kuisimika miti ya mianzi katika sakafu ya chumba hicho ambayo ilikuwa bado haijasakafiwa.
Kilikuwa ni kibanda cha hali ya chini lakini penzi lao lilikifanya kibanda hicho kiwe kama vile kasri ya mfalme na malkia.
Ilimgharimu mwezi mzima, Wakati kurudi kati hali ya kawaida, alitakiwa kukubaliana na kila kitu, ya kwamba bibi yake amekwenda. Alitakiwa kendelea na shughuli zake katika kibanda chake cha kuchomea kiti moto kilichokuwa njia panda ya shule ya sekondari  lufilyo, shule ambayo Pendo anasoma.
Ni katika kibanda hicho ndipo kila kitu kuhusu uhusiano wao kilipoanzia, ilikuwa siku ambayo wote wawili kamwe haitoki katika kichwa chao, siku hiyo ambayo  pendo aliingia na rafiki zake katika kibanda hicho  kwa mara ya kwanza, na walifika hapo kupata kitimoto kama wateja wengine lakini pale macho yao walipogongana pendo aliona kila kitu ambacho huwa alikuwa akikisikia shuleni kutoka kwa wasichana wenzake, ni kweli alikuwa mvulana mzuri kama vile ambavyo kila mmoja alisema , na ni kweli kibanda chake kilikuwa kimejaa wateja wa jinsia ya kike, wanafunzi hao walikuwa wakila kiti moto pamoja na ndizi huku kila mmoja akitaka kuongea neno lolote na wakati , yalikuwa mambo mengi yaliyowavutia wasichana hawa lakini zaidi ni upole wake , ukarimu wake na vile alivyokuwa shapu kumjali kila mmoja.
“naitwa pendo.”
Aliongea pendo kwa sauti yake laini huku uso wake ukiwa na tabasamu, macho yake yalikuwa juu ya macho ya Wakati na yeye alikuwa ametabasamu pia. Japo hili tabasamu halikuwa sawa na tabasamu lolote ambalo liliwahi kuonekana kwenye uso wake.
“sijawahi kukuona hapa, wewe ni mgeni?”
Aliongea wakati huku akiwa bado amesimama , kwenye meza hiyo.
“hey, waka mpenzi , niongeze kachumbari.”
Aliongea msichana , mmoja aliyekuwa ameketi meza ya tatu toka pale .
“usijali jeni nakuongeza ngoja nichukue oda hapa.”
Aliongea wakati , wala hakugeuza macho yake kumuangalia msichana huyo , bado macho yake yalitaka kuuuona uso wa pendo pekee na kujua zaidi kumhusu.
“Ni mgeni ndio , baba yangu ameamishiwa hapa kikazi.”
Aliongea pendo.
‘ni daktari?”
Aliuliza
“ndio , kwa nini?”
“nafikiri nina mjua , niliongea na daktari mpya wiki mbili zilizopita , alinitaka nimpelekee kiti moto nyumbani kwake.”
Aliongea wakati.
“ni kitu gani kimekufanya ufikiri ni baba yangu?”
Aliuliza .
“namjua kila mtabibu anayefanya kazi katika hospitali ya itete , huu ni mji mdogo pendo.”
Aliongea wakati huku akitabasamu.
Itaendelea kesho, pia unaweza kusoma stori sehemu ya mbele ya stori hii zaidi ya vitabu 6 vipo hewani sasa, pia unaweza kujipatia vitabu vyetu vingine kwa bei ya nafuu, kuna ofa ya vitabu kwa whatsap na inbox fb, viwili sh 1700 vitatu sh 2400
vinne sh 3200 vitano sh 4000,kimoja sh 1000.
Stori zetu zingine ni hizi zifuatazo:
NOT YOU NOW book 1 – 24 , MTOTO WA MTAA BOOK 1 – 20, I WILL HUNT YOU DOWN 1&2, WHEN I  SAY I LOVE 1 – 9, KIMBIA MPENZI BOOK 1,2,3,4,5 NA 6.  YOU CAN’T MAKE ME A FOOL AGAIN, SISTAHILI KUFUNGWA, NAIPENDA TANZANIA.
CHANGUO NGUO book01,02,03
TEKETEKE TAMU BOOK 01,02
YES BOSS BOOK 1,2, ASMA KIDOTI book 1,2,3 MSICHANA NYUMBA YA PILI BOOK1,2, KOCHA WA TENESI BOOK1,2, PITISHA KWENYE  MPASUO, WEZELE,
TWAMTOA MWARI book 1,2,
MCHEPUKO WA MSHUA, KITAA FLANI, MSAGAJI,
TAXI BUBU,
MAMA WA KAMBO BOOK 1,2,
DEMU WA GEREJI, MZEE WA CHUMVINI,
NATAKA ZOTE,
NIPE UTAMU KAKA JAMBAZI,
zamu zamu, OPARESHENI MAPENZI BOOK 1,2 JIRANI NYAMA YA HAMU BOOOK 1,2,3,4,5,6,7 NJOO MAMA HAYUPO 1,2,3,4,5,6 NATAKA UNIFUATE KICHAKANI BOOK 1,2,3,4,5 AISHA CHA UTAMU BOOK 1,2,3,4,5 KIDOLE AKINITOSHI BOOK 1,2,3  BEKI TATU WA MTAA BOOK 1,2,3,4
THE AFRICAN SEX MASHINE BOOK 1,2,3,4,5 na 6 KARIBU KITAA TICHA BOOK 
1,2,3,4,5 , KWAYA MASTA BOOK 1 , 2, 3 na 4 WIFI NIPE UTAMU … KAKA HAYUPO BOOK 1,2&3,4,5,6,7 , SHUGA MUMY LA 
KISTASHA BOOK 1,2,3. MUUZA MAZIWA BOOK 1- 16 , TOTO LA KISHUA 1- 9 , SI UNA MATE NIMEKUSIA BOOK 1 – 5,HALO HALO 1-9 JIMAMA MTAA WA PILI 1 -8
Namba zinazotumika kwa ajili ya malipo ni mpesa 0757 414 436 , tigo pesa 0715 557 191 airtel money 0789117674
Namba zote zimesajiliwa kwa jina la Deogratius Lwasye

No comments: