Tume
ya taifa ya uchaguzi NEC imesema haina mpango wa kusogeza mbele
uchaguzi mkuu wa rais na wabunge kutokana na uwezekano wa kutokamilika
kwa daftari la kudumu la wapiga kura.Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji
mstaafu Damian Lubuva ameyasema hayo jijini dar es salaam ambapo amesema
tume imepokea BVR 248 na kufanya jumla ya mashine hizo kufikia 498 na
kuongeza kuwa muda mfupi ujao watapokea nyingine 1600 zinazowasili kwa
ndege ya kukodi kutoka Dubai.
Aidha jaji lubuva ametaja awamu ya
pili ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura
itaendelea April 24 mwaka huu, siku ambayo pia watapokea BVR nyingine
1600 ambazo amesema zitaharakisha kasi ya uandikishaji kwani wataweza
kuandikisha mikoa mingi kwa wakati mmoja na kuongeza kuwa awamu ya pili
ya zoezi la BVR itakuwa mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Iringa.
Kwa upande wake naibu katibu mkuu kitengo cha daftari la wapiga kura Sisti Karia amesema endapo wangekuwa na mashine za bvr za kutosha wangezigawa kwenye halmashauri nchi nzima hivyo wangeweza kuendesha zoezi la kuandikisha watu kwa siku 28 tu nchi nzima.(KILONGE)

No comments:
Post a Comment