Tuesday 13 March 2018

KIMBIA MPENZI TUTAKUTANA MBELE KWA MBELE!!(Sehemu ya 4)


                                                    (the first run away love to told by Deogratius gift kipapa.)
EPISODI 04
INTRO:
Simulizi ya msichana wa shule aliyelazimika kumtorosha mpenzi wake mbali na baba yake pamoja na serikali mara baada ya kumpa ujauzito. Kamwe hakufikiri kwamba kumruhusu akimbie ni kuliruhusu penzi lake lipotelee mbali milele.  Simulizi hii, haitakuonyesha ni jinsi gani ilivyo kutengana na mpenzi wako pekee bali pia itakushangaza zaidi na uhusiano wa baba na mwana ambao kamwe hukuwahi kuuvutia picha, kuna machozi, na jasho, mbio na kuvuta pumzi, kama ulisoma simulizi yoyote ya mapenzi kutoka kwa gift kipapa na kuhakikishia ya kwamba haujasoma kitu. This is not just a heart to heart story but I run away love which no one could never ever found.
ILIPOISHIA EPISODI 03….
Walikumbatiana na kulia kwa pamoja , kwa muda huo mfupi walijisahau kwamba hapo walipo sio sehemu ya kujiachia kiasi hicho , ilikuwa ni ofisi na huenda wakati wowote watu wanaweza kufika hapo.
“twende nyumbani kwako, unatakiwa kujiandaaa sasa hivi, hatuwezi jua habari zinasambaa sana hapa itete.”
Aliongea pendo na kisha wote waliamka, nyumbani kwa wakati hakukuwa mbali sana kutokea hapo iliwachukua nusu saa tu kufika na haraka wakati alinza kuhangaika na nguo zake na vitu vingine ambavyo kwake vilikuwa na umuhimu.
“umeshachagua sehemu ya kwenda?”
Aliuliza pendo.
MWENDELEZO WAKE:
‘nini?”
Aliuliza wakati kwa mshtuko kwa kweli hilo lilikuwa jambo ambalo hadi wakati huo alikuwa bado ajalipangilia , alichojua yeye ni kwamba anatakiwa kukimbia.
“sehemu ya kwenda , arusha mwanza , morogoro dar es salaam , iringa, bu..”
Aliuliza pendo.
“dar es salam , kila mtu anasema maisha ni mazuri huko , ajira za kumwaga na watu wala hawafuatiliani kama hapa itete , askari hawataweza kunipata.”
Aliongea wakati .
“sawa dar pazuri , hata mimi ningekushauri huko.”
Aliongea pendo kisha wote walicheka, dar es salaam ilikuwa sehemu ambayo, ilikuwa ikizungumziwa zaidi na kila mtu hapo kwa umashuhuri wake.
***
Pendo aliondoka na kumuacha wakati peke yake akiendelea kuandaa vitu vyake, lakini hiyo ilikuwa nafasi ya kumfanya wakati anaanze kulia tena, machoizi yote aliyokuwa nayo yalirudia tena , alikuwa akilia zaidi hata ya vile alivyokuwa akili kwenye msiba wa bibi yake , kwa kweli kutengena na pendo lilikuwa ni jambo lililomogopesha sana katika maisha yake, alitamamani kama kungekuwa na njia yoyote ile angeweza kuitumia lakini sio hiyo ya kutengana na pendo, msichana huyu alikuwa ni tumaini lake pekee.
“mbona hivyo tena jamani, inamaana utakuwa unalia hivyo muda wote huko uendako, tafadhari jikaze mpenzi.”
Aliongea pendo mara baada ya kuingia kwenye nyumba hiyo na kumkuta wakati akiwa wameketi chini akilia .
“kwa kweli siwezi , siwezi mpenzi , siwezi kuishi maisha haya.”
Aliongea wakati huku akilia, pendo alimnyanyua toka pale chini na kumkumbatia , alijaribu kumtuliza lakini kila kitu kilibadilika pale yeye mwenyewe alipojaribu kulivutia hisia suala hilo , wakaishia kulia wote muda wote , na waliponyamaza, ilibidi wafanye vyote pamoja, kila kitu kilingizwa kwenye begi dogo la mgongoni ambalo pendo alikuwa akilitumia kubebea madaftari shule, alimfungia chakula pamoja na kiasi Fulani cha pesa alichokichukua kwenye kabati la baba yake pamoja na akiba yajke binafsi, alijua wakati anahitaji pesa kwa muda huo kuliko kitu chochote .
“ahsante mpenzi.”
Aliongea wakati.
“karibu mpenzi , oh alafu chakula usikifungue sasa hivi , nataka mpaka ukiwa ndani ya basi , nataka ule ukiwa unakikumbuka kwamba ndio chakula chako cha mwisho kula kutoka kwangu.”
Aliongea pendo na kisha kutoa tabasamu dogo usoni kwake. Wakati hakujibu kitu zaidi ya kumkumbatia.
“huko tayari kwa kuondoka?”
“sasa hivi? Hapa itete hamna basi  linalo toka nje ya mjini muda huu.”
“najua , itabidi ukapandie lwangwa, kama ukiendelea kuwa hapa hadi wazazi wangu watapojua kila kitu tutakuwa tumeshachelewa kabisa.”
Aliongea pendo.
“sawa mpenzi.”
Wakati aliitikia na kisha kwa pamoja walitoka nje ya kibanda hicho, aligeuka nyuma na kukiangalia kwa mara ya mwisho, moyo wake uliuma kuona anakimbia nyumba aliyoijenga mwenyewe, eneo hilo lilikuwa kamili kwake, furaha aliyokuwa anaipata ndani ya kibanda hicho akiwa na mpenzi wake ilikuwa na maana ya maisha kwake,.

  Walianza kutembea huku wakiwa wameshikana mikono, njia waliyopita ilikuwa ni ya vichochoro, hawakutaka kukutana na watu na kuwaangalia jinsi walivyokuwa na huzuni muda wote.
Kila kitu kilikuwa kigumu kwao kwa kweli walitamani kubadilisha kila kitu lakini hilo lilikuwa juu ya uwezo wao .
Iliwachukua muda kidogo kuufikia mji wa lwangwa , ulikuwa ni mji mdogo lakini ulikuwa na kelele na vurugu za kila aina katika soko lake ambalo lilikuwa limejaa bidhaa za kila aina.
Wakulima wa ndizi walikuwa wamesimama nyuma ya mikungu yao na kumuita yoyote Aliyepita karibu yao ili anunue japo hata kichanja kimoja cha mkungu huo .
Sehemu ya matunda hali nayo ilikuwa hivyo hivyo maparachichi, maembe yalikuwa yamejaa kwenye meza , na wauzaji walikuwa wakipiga kelele muda wote kumuita yoyote.
Wakati pamoja na pendo walitakiwa kupita kati kati yao, walivutwa mkono na baadhi ya wauzaji hao waliokuwa wakisisitiza kununuliwa kwa bidhaa zao , lakini walibaki kimya.
Angalia , wakati , basi la sikutegemea! na tena limebaki peke yake.”
Aliongea pendo huku akionyesha basi kubwa lililokuwa lkimeegeshwa kwenye stendi ya mji huo likiwa na maandishi makubwa yaliyoandikwa ‘sikutegemea trans’  kwenye ubavu wake.
Itaendelea kesho, pia unaweza kusoma stori sehemu ya mbele ya stori hii zaidi ya episodi 50 zipo tayari, pia unaweza kujipatia vitabu vyetu vingine kwa bei ya nafuu, kuna ofa ya vitabu kwa whatsap na inbox fb, viwili sh 1700 vitatu sh 2400
vinne sh 3200 vitano sh 4000,kimoja sh 1000.
Stori zetu zingine ni hizi zifuatazo:
NOT YOU NOW book 1 – 24 , MTOTO WA MTAA BOOK 1 – 20, I WILL HUNT YOU DOWN 1&2, WHEN I  SAY I LOVE 1 – 9, KIMBIA MPENZI BOOK 1,2,3,4,5 NA 6.  YOU CAN’T MAKE ME A FOOL AGAIN, SISTAHILI KUFUNGWA, NAIPENDA TANZANIA.
BABA WA KAMBO book01,
CHANGUO NGUO book01,02,03
TEKETEKE TAMU BOOK 01,02
YES BOSS BOOK 1,2, ASMA KIDOTI book 1,2,3 MSICHANA NYUMBA YA PILI BOOK1,2, KOCHA WA TENESI BOOK1,2, PITISHA KWENYE  MPASUO, WEZELE,
TWAMTOA MWARI book 1,2,
MCHEPUKO WA MSHUA, KITAA FLANI, MSAGAJI,
TAXI BUBU,
MAMA WA KAMBO BOOK 1,2,
DEMU WA GEREJI, MZEE WA CHUMVINI,
NATAKA ZOTE,
NIPE UTAMU KAKA JAMBAZI,
zamu zamu, OPARESHENI MAPENZI BOOK 1,2 JIRANI NYAMA YA HAMU BOOOK 1,2,3,4,5,6,7 NJOO MAMA HAYUPO 1,2,3,4,5,6 NATAKA UNIFUATE KICHAKANI BOOK 1,2,3,4,5 AISHA CHA UTAMU BOOK 1,2,3,4,5 KIDOLE AKINITOSHI BOOK 1,2,3  BEKI TATU WA MTAA BOOK 1,2,3,4
THE AFRICAN SEX MASHINE BOOK 1,2,3,4,5 na 6 KARIBU KITAA TICHA BOOK 
1,2,3,4,5 , KWAYA MASTA BOOK 1 , 2, 3 na 4 WIFI NIPE UTAMU … KAKA HAYUPO BOOK 1,2&3,4,5,6,7 , SHUGA MUMY LA 
KISTASHA BOOK 1,2,3. MUUZA MAZIWA BOOK 1- 16 , TOTO LA KISHUA 1- 9 , SI UNA MATE NIMEKUSIA BOOK 1 – 5,HALO HALO 1-9 JIMAMA MTAA WA PILI 1 -8
Namba zinazotumika kwa ajili ya malipo ni mpesa 0757 414 436 , tigo pesa 0715 557 191 airtel money 0789117674
Namba zote zimesajiliwa kwa jina la Deogratius Lwasye

No comments: