Tuesday 13 March 2018

KIMBIA MPENZI TUTAKUTANA MBELE KWA MBELE!!(Sehemu ya 3)


                                                    (the first run away love to told by Deogratius gift kipapa.)
EPISODI 03
INTRO:
Simulizi ya msichana wa shule aliyelazimika kumtorosha mpenzi wake mbali na baba yake pamoja na serikali mara baada ya kumpa ujauzito. Kamwe hakufikiri kwamba kumruhusu akimbie ni kuliruhusu penzi lake lipotelee mbali milele.  Simulizi hii, haitakuonyesha ni jinsi gani ilivyo kutengana na mpenzi wako pekee bali pia itakushangaza zaidi na uhusiano wa baba na mwana ambao kamwe hukuwahi kuuvutia picha, kuna machozi, na jasho, mbio na kuvuta pumzi, kama ulisoma simulizi yoyote ya mapenzi kutoka kwa gift kipapa na kuhakikishia ya kwamba haujasoma kitu. This is not just a heart to heart story but I run away love which no one could never ever found.
ILIPOISHIA EPISODI 02….
“hilo litawezekana vipi pendo , wamesha kufukuza shule tayari , na wakati wowote askari watatumwa kuja kunisaka , yote haya yamekwisha pendo , yamekwisha , kila kitu kinakufa baada ya bibi kufa , labda kwa sababu yeye ndio mtu pekee aliyekuwa anajua siri ya penzi letu , hivyo kwa kuwa amekufa basi kila kitu kina kuwa wazi , ninaogopa sana pendo , unamjua baba yako, hawezi kuniacha, amekuwa akiwa piga watu ambao wanakuongelesha tu njiani je vipi kuhusu mimi niliye kupa mimba kabisa?”
Aliongea wakati huku akilia.
MWENDELEZO WAKE:
“hapana , hapana , mpenzi, baba yangu hawezi kukufikia , siwezi kumruhusu akuguse, siwezi.”
Aliongea pendo kwa ujasili , alikuwa amejikaza, sura yake ya unyonge yote ilipotea.
“tutafanya nini , hata ukisema hautanitaja, kila mtu ameona jinsi nilivyokukumbatia pale nje, hakuna siri tena pendo , tumepoteza kila kitu.”
Aliongea wakati huku akiendelea kulia muda wote.
“unatakiwa kukimbia!”
Aliongea pendo na kumfanya wakarti ashtuke.
“nini!?”
“hakuna namna , wakati , hiyo ndio njia pekee ya wewe kuendelea kuwa salama unaweza kwenda popote ambapo hakuna anaye kufahamu , na harafu utarudi pale kila kitu kitakapotulia , au tutakutana mbele kwa mbele.”
Aliongea pendo.
“hapana pendo , siwezi kwenda popote nikakuacha wewe nyuma , nakuhitaji pendo, wewe ndio kila kitu kwangu , ninakwambia maneno haya kila siku.”
“najua hata mimi siwezi kubaki peke yangu bila wewe , lakini tunatakiwa kukabiliana na hii hali.’
Aliongea pendo.
“basi tukimbie wote mpenzi.’
Aliongea wakati.
“hapana hilo haliwezekani, natakiwa kubaki, umesahau kwamba mimi ni mjamzito, natakiwa kuwa mahali salama, ili nijifungue salama, unajua baba yangu jinsi anavyonipenda , atafoka na kunipiga ndani ya siku kadhaa lakini baada ya muda kila kitu atakisahau na kisha atanitafutia shule nyingine  na nitajifungua salama , nitaendelea kupigania ndoto yetu , wakati wewe huko ukitafuta kwa njia yoyote uutakayokutana nayo , na utarejea wakati hasira za baba yangu zimesha kwisha.”
Aliongea  pendo huku akimuangalia wakati usoni, kuna kitu kimoja pendo alishindwa kukielewa kabisa, wakati wala hakuwa anahofia juu ya baba yake pamoja na kukamatwa na polisi kama ambavyo alikuwa anahofia kumpoteza, alikuwa anampenda pendo kupita kiasi na alitaka kuwa nae katika kipindi chote cha maisha yake, lakini hili wazo la kukimbia lina kwenda kuzipoteza  nafasi zote za kuwa karibu na pendo alizokuwa nazo, na hilo ndilo lilikuwa likimpa hofu kupita kiasi ni kama vile mbele yake kila kitu kilitoweka hata mwanga na kubaki giza nene ambalo lilikuwa halimpi nafasi ya kujua hata kitu kilicho sentimita tatu kutoka alipo kina muonekano gani.
“tafadhari pendo , siwezi kufanya hili , siwezi kukaa mbali na wewe hata kidogo , nitakufa , nitakufa mimi.”
Aliongea wakati huku akilia , kichwa chake kilikuwa kimeegamia kwenye kifua cha pendo.
‘najua wakati , najua mpenzi wangu , lakini hatuwezi kukabiliana na lolote lililo mbele yetu , kila kitu kina kwenda kuwa kigumu, kama hauta kubali kukaa mbali na mimi sasa hivi , serikali itatutenga milele, miaka thelathini ni mingi wakati , sitaweza kuishi miaka yote hiyo bila kuigusa ngozi yako, hapana, nitaumia sana.”
Aliongea pendo na maneno yake yalimgusa wakati kupita kiasi , alielewa ya kwamba kwamba kama akitaka kwenda kinyume na wazo la pendo ataliweka penzi lao kwenye hatari hata zaidi.
“sawa , sawa mpenzi , nitakwenda, nitakimbia.’
Aliongea wakati na kumfanya pendo alie , alipaswa kutabasamu baada ya wakati kukubaliana na wazo lake lakini alipofikiria juu ya upweke atakaokwenda kukabiliana nao alijikuta anapata maumivu makali sana moyoni.
Walikumbatiana na kulia kwa pamoja , kwa muda huo mfupi walijisahau kwamba hapo walipo sio sehemu ya kujiachia kiasi hicho , ilikuwa ni ofisi na huenda wakati wowote watu wanaweza kufika hapo.
“twende nyumbani kwako, unatakiwa kujiandaaa sasa hivi, hatuwezi jua habari zinasambaa sana hapa itete.”
Aliongea pendo na kisha wote waliamka, nyumbani kwa wakati hakukuwa mbali sana kutokea hapo iliwachukua nusu saa tu kufika na haraka wakati alinza kuhangaika na nguo zake na vitu vingine ambavyo kwake vilikuwa na umuhimu.
“umeshachagua sehemu ya kwenda?”
Aliuliza pendo.
Itaendelea kesho, pia unaweza kusoma stori sehemu ya mbele ya stori hii zaidi ya episodi 50 zipo tayari, pia unaweza kujipatia vitabu vyetu vingine kwa bei ya nafuu, kuna ofa ya vitabu kwa whatsap na inbox fb, viwili sh 1700 vitatu sh 2400
vinne sh 3200 vitano sh 4000,kimoja sh 1000.
Stori zetu zingine ni hizi zifuatazo:
NOT YOU NOW book 1 – 24 , MTOTO WA MTAA BOOK 1 – 20, I WILL HUNT YOU DOWN 1&2, WHEN I  SAY I LOVE 1 – 9, KIMBIA MPENZI BOOK 1,2,3,4,5 NA 6.  YOU CAN’T MAKE ME A FOOL AGAIN, SISTAHILI KUFUNGWA, NAIPENDA TANZANIA.
BABA WA KAMBO book01,
CHANGUO NGUO book01,02,03
TEKETEKE TAMU BOOK 01,02
YES BOSS BOOK 1,2, ASMA KIDOTI book 1,2,3 MSICHANA NYUMBA YA PILI BOOK1,2, KOCHA WA TENESI BOOK1,2, PITISHA KWENYE  MPASUO, WEZELE,
TWAMTOA MWARI book 1,2,
MCHEPUKO WA MSHUA, KITAA FLANI, MSAGAJI,
TAXI BUBU,
MAMA WA KAMBO BOOK 1,2,
DEMU WA GEREJI, MZEE WA CHUMVINI,
NATAKA ZOTE,
NIPE UTAMU KAKA JAMBAZI,
zamu zamu, OPARESHENI MAPENZI BOOK 1,2 JIRANI NYAMA YA HAMU BOOOK 1,2,3,4,5,6,7 NJOO MAMA HAYUPO 1,2,3,4,5,6 NATAKA UNIFUATE KICHAKANI BOOK 1,2,3,4,5 AISHA CHA UTAMU BOOK 1,2,3,4,5 KIDOLE AKINITOSHI BOOK 1,2,3  BEKI TATU WA MTAA BOOK 1,2,3,4
THE AFRICAN SEX MASHINE BOOK 1,2,3,4,5 na 6 KARIBU KITAA TICHA BOOK 
1,2,3,4,5 , KWAYA MASTA BOOK 1 , 2, 3 na 4 WIFI NIPE UTAMU … KAKA HAYUPO BOOK 1,2&3,4,5,6,7 , SHUGA MUMY LA 
KISTASHA BOOK 1,2,3. MUUZA MAZIWA BOOK 1- 16 , TOTO LA KISHUA 1- 9 , SI UNA MATE NIMEKUSIA BOOK 1 – 5,HALO HALO 1-9 JIMAMA MTAA WA PILI 1 -8
Namba zinazotumika kwa ajili ya malipo ni mpesa 0757 414 436 , tigo pesa 0715 557 191 airtel money 0789117674
Namba zote zimesajiliwa kwa jina la Deogratius Lwasye

No comments: