Monday 26 March 2018

KIMBIA MPENZI TUTAKUTANA MBELE KWA MBELE!! (Sehemu ya 10)


                                                    (the first run away love to told by Deogratius gift kipapa.)
EPISODI 10
INTRO:
Simulizi ya msichana wa shule aliyelazimika kumtorosha mpenzi wake mbali na baba yake pamoja na serikali mara baada ya kumpa ujauzito. Kamwe hakufikiri kwamba kumruhusu akimbie ni kuliruhusu penzi lake lipotelee mbali milele.  Simulizi hii, haitakuonyesha ni jinsi gani ilivyo kutengana na mpenzi wako pekee bali pia itakushangaza zaidi na uhusiano wa baba na mwana ambao kamwe hukuwahi kuuvutia picha, kuna machozi, na jasho, mbio na kuvuta pumzi, kama ulisoma simulizi yoyote ya mapenzi kutoka kwa gift kipapa na kuhakikishia ya kwamba haujasoma kitu. This is not just a heart to heart story but I run away love which no one could never ever found.
ILIPOISHIA EPISODI 9….
“mambo ona! ona, mama ameninunulia kuku!”
Aliongea mtoto huyo mara baada ya kuingia na kuketi na mama yake , mikono yake ilikuwa imelishikilia paja la kuku  alilokuwa ameanza kulitafuna toka huko nje.
“oh , mama mzuri , kuku na nini?”
Aliuliza .
“na chips.”
Aliongea mtoto huyo huku akitabasamu.
“oh safi sana , mwambie ahsante mama.”
“ahsante mama.’
Mtoto huyo aliongea huku akimuangalia mama yake usoni.
MWENDELEZO WAKE:

“haya tulia ule  kwanza acha kuongea ongea umesikia.”
Aliongea mama yake.
‘sawa mama.”
Aliiitikia mtoto huyo nakuendelea kulila paja lake la kuku.
Wakati nae aliendelea kula chapati zake, dakika kumi na tano baadae basi lilianza kuondoka tena, ilikuwa misitu , milima na mabonde , basi hilo lilipita kote huko huku picha za muziki wa bongo fleva zikionekana katika LCD zilizofungwa katika basi hilo.
***
Yalikuwa ni majira ya saa nane za usiku, mzee fanuel na mkewe bado walikuwa hawajalala, kila kitu kilichotokea siku hiyo  kwake kilikuwa kama ndoto ya kutisha , kwa kweli hadi wakati huo hakuwa tayari kuukubali ukweli ya kwamba kirahisi namna hiyo binti yake amepewa ujauzito na mhusika amepotelea kusiko julikana.
“siwezi kukubali , siwezi, siwezi hata kidogo.”
Aliongea fanuel akiwa bado hajatulia kabisa.
“itabidi tukubali mume wangu , unafikiri tutafanyaje sasa?”
Aliongea mkewe kwa sauti ya upole , kwa muda huo alikuwa anahofia kila kitu, katika maisha yake yote ya ndoa kamwe hakuwa hi kumuona mumewe akiwa katika hali hiyo.
“lazima tuitoe hiyo mimba.”
Aliongea kauli hiyo iliyomshtua mkewe kupita kiasi.
“nini?”
Aliuliza mkewe kwa mshangao , kwa kweli hakutegemea kauli hiyo ingetoka kwa mumewe, alijua jinsi anavyompenda binti yao , uamuzi wa kuhatarisha maisha yake kamwe usingetoka kinywani mwake.
“hakuna njia nyingine , kila mtu anajua jinsi nilivyokuwa jirani na yule kijana , amenifanya mjinga , unafikiri ninaweza kuruhusu binti yangu azae mtoto wake na itete nzima inicheke , hilo haliwezi kutokea , huyo hawezi kuwa mimi.”
Aliongea mzee fanuel kwa msisitizo.
“fanuel , unaongelea juu ya maisha ya binti yetu hapa.”
Aliongea mkewe huku akimuangalia mumewe usoni.
“nina madaktari bora, sitarajii makosa yoyote, wamekuwa wakifanya kazi hii kwa miaka na miaka.”
Aliongea mzee fanuel.
“hapana fanuel hausemi kweli , niambie kwamba unafanya mzaha, hauendi kuyatia maisha ya binti yetu hatarini.”
Aliongea mkewe huku akimuangalia usoni , macho yake aliyakaza na alikuwa anaamani yanaweza kumshawishi mumewe  kama wakati wa nyuma.
“sio kwa huu upuuuzi alioufanya, siwezi kuruhusu mimba hiyo ikiue , utanisamehe anna.”
Aliongea kwa msisitizo huku akilitaja jina la mkewe, hiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kumuita jina lake halisi kwa kipindi chote cha ndoa yao  na hili lilimsibitishia ya kwamba mwanaume huyu hana mzaha hata kidogo.
“hapana , hapana fanuel maisha…”
Alijaribu kuongea lakini kofi zito lililotua usoni kwake lilimfanya asitishe kauli yake , alijaribu kuongea tena kofi lingine lilitua usoni kwake, linguine na lingine, lakini hakuna hata kofi moja lililomfanya aufunge mdomo wake , bado alitaka kuongea lolote , bado alikuwa anaamini maneno yake yanaweza kubadili fikra za mumewe usiku huo na hatimaye kuokoa maisha ya binti yake , lakini hakuna mafiniko aliyoyapata zaidi ya kuendelea kupata makofi mfululizo.
Wakati ugomvi huu mzito kuwahi kutokea katika familia hiyo unaendelea , Pendo alikuwa mlangoni ameketi chini akilia , alikuwa hapo usiku wote sababu alijua lazima wazazi wake watalijadili suala lake na alihitaji kujua ni nini hasa wanachofikiria juu ya jambo hilo na sasa  jibu ambalo amelipata toka kwa baba yake lilimfanya ajikute analia muda wote , na huu ugomvi ulioibuka kati yao ndio ulimfanya achanganyikiwe kabisa , kwa mara ya kwanza katika maisha yake vitendo vyake vimeharibu amani yote iliyokuwa kama lulu katika familia yake.
Na hili wazo la baba yake kuutoa ujauzito wa mwanaume aliyempenda kuliko kila kitu katika maisha yake , lilimfaya ajue kwamba tangu sasa nyumbani kwao sio sehemu salama kwake tena , alijilaumu kwa kupuuzia wazo la kutoroka pamoja na wakati , alimsihi wafanye hivyo lakini yeye alikuwa anatumaini na wazazi wake na sasa kila kitu kimeonekana dhahiri.
“itabidi na mimi  nikimbie.”
Aliwaza  na muda huo huo aliamka mlangoni hapo na kuelekea chumbani kwake , kilichofuata ilikuwa ni kuchukua vitu vyake muhimu haraka , alipofika kwenye droo yake ya pesa alijikuta ananyong’onyea baada ya kukumbuka ya kwamba zote alisha mpa wakati .
Lakini ghafla alitabasamu mara baada ya kukumbuka jambo Fulani , alielekea jikoni haraka na kuchukua kibubu kilichokuwa kimefichwa ndani ya kabati , nyuma ya makopo ya viungo vya kupikia , kilikuwa kibubu cha mama yake , alikificha sababu alitaka kukusanya pesa za kwa siri bila ya mumewe kujua, pesa hizo zilkuwa ni kwa ajili ya kumnunulia mumewe zawadi ya birthday  itakayomshangaza zaidi kwa mara ya kwanza katika maisha yao.
“happy birth day baba.”
Aliongea pendo nakisha kufungua kufuli la kibubu hicho, aliingia mikono yake na kuchukua kila noti iliyokuwemo humo , zote. Mkono wake ulikuwa umejaa noti hizo zilizokuwa kiholela na kisha kuzipanga , alirejea chumbani kwake na akakiangalia chumba hicho kwa mara ya mwisho.
“nitavikumbuka vitu vyangu.”
Aliwaza na kisha kuanza kutembea , hakufika popote akasimama kama vile amebadili wazo na kisha akaenda kwenye meza yake ya kusomea haraka, alifungua droo na kuchukua peni na karatasi , aligundua ya kwamba haitakuwa busara kama akitoka katika nyumba hiyo , bila kuacha ujumbe wowote kwa wazazi wake.
Alikuwa anaandika ujumbe huo huku akilia kwa uchungu, kwenda mbali na wazazi wake halikuwa jambo ambalo alikuwa anataka limtokee , alikuwa anawapenda mno , lakini wazo la baba yake la kutaka aitoe mimba ya mwanaume anayempenda lilimfanya asibaki na namna yoyote ile , ilimbidi akimbie na kukaa mbali na baba yake mpaka mtoto atakapo zaliwa  na labda kuanzia hapo ataweza kuelewa.
       “nakuja kwako , wakati , natuamaini tutakutana mpenzi wangu , na tutaishi maisha mazuri huko.”
Aliwaza pendo huku akitembea , kuelekea ilipo stendi ya mji huo, tayari ilikuwa imetimia mida ya saa kumi za alfajiri , na huo ulikuwa muda  muafaka kwa magari kuondoka kuelekea mji wa tukuyu.
Aliyakuta magari mawili na yote yalikuwa na abiria kadhaa , aliingia kwenye moja wapo na dakika kumi na tano baadae gari hilo lilianza kuondoka katika eneo hilo , na hiyo ilikuwa kwa heri ya pendo wa mji wa itete na kwa wazazi wake pia.
Itaendelea kesho, pia unaweza kusoma stori sehemu ya mbele ya stori hii zaidi ya episodi 50 zipo tayari, pia unaweza kujipatia vitabu vyetu vingine kwa bei ya nafuu, kuna ofa ya vitabu kwa whatsap na inbox fb, viwili sh 1700 vitatu sh 2400
vinne sh 3200 vitano sh 4000,kimoja sh 1000.
Stori zetu zingine ni hizi zifuatazo:
NOT YOU NOW book 1 – 24 , MTOTO WA MTAA BOOK 1 – 20, I WILL HUNT YOU DOWN 1&2, WHEN I  SAY I LOVE 1 – 9, KIMBIA MPENZI BOOK 1,2,3,4,5 NA 6.  YOU CAN’T MAKE ME A FOOL AGAIN, SISTAHILI KUFUNGWA, NAIPENDA TANZANIA.
BABA WA KAMBO book01,02,03,
CHANGUO NGUO book01,02,03
TEKETEKE TAMU BOOK 01,02
YES BOSS BOOK 1,2, ASMA KIDOTI book 1,2,3 MSICHANA NYUMBA YA PILI BOOK1,2, KOCHA WA TENESI BOOK1,2, PITISHA KWENYE  MPASUO, WEZELE,
TWAMTOA MWARI book 1,2,
MCHEPUKO WA MSHUA, KITAA FLANI, MSAGAJI,
TAXI BUBU,
MAMA WA KAMBO BOOK 1,2,
DEMU WA GEREJI, MZEE WA CHUMVINI,
NATAKA ZOTE,
NIPE UTAMU KAKA JAMBAZI,
zamu zamu, OPARESHENI MAPENZI BOOK 1,2 JIRANI NYAMA YA HAMU BOOOK 1,2,3,4,5,6,7 NJOO MAMA HAYUPO 1,2,3,4,5,6 NATAKA UNIFUATE KICHAKANI BOOK 1,2,3,4,5 AISHA CHA UTAMU BOOK 1,2,3,4,5 KIDOLE AKINITOSHI BOOK 1,2,3  BEKI TATU WA MTAA BOOK 1,2,3,4
THE AFRICAN SEX MASHINE BOOK 1,2,3,4,5 na 6 KARIBU KITAA TICHA BOOK 
1,2,3,4,5 , KWAYA MASTA BOOK 1 , 2, 3 na 4 WIFI NIPE UTAMU … KAKA HAYUPO BOOK 1,2&3,4,5,6,7,  SHUGA MUMY LA 
KITASHA BOOK 1,2,3. MUUZA MAZIWA BOOK 1- 16, TOTO LA KISHUA 1- 9, SI UNA MATE NIMEKUSIA BOOK 1 – 5, HALO HALO 1-9, JIMAMA MTAA WA PILI 1 -8,
Namba zinazotumika kwa ajili ya malipo ni mpesa 0757 414 436 , tigo pesa 0715 557 191 airtel money 0789117674
Namba zote zimesajiliwa kwa jina la Deogratius Lwasye.

No comments: