Wanachama
wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram nchini Nigeria,
wameshambulia vijiji vya kaskazini mwa Cameroon na kuua watu wasiopungua
10 na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Watu walioshuhudia wanasema kuwa,
wanachama wa kundi hilo walitekeleza kwa pamoja hujuma hiyo asubuhi ya
siku ya Ijumaa dhidi ya vijiji vya Biya na Bolabari katika eneo la
Kolowata kaskazini mwa nchi hiyo.
Inaelezwa kuwa, wanachama wa kundi
hilo la kitakfiri walikimbilia Nigeria kupitia mpaka wa pamoja, baada ya
majeshi ya serikali ya Cameroon kuwasili eneo la tukio.
Nigeria ndio
makao makuu ya kundi la Boko Haram, hata hivyo wanachama wake wamekuwa
wakivuka mipaka ya nchi hiyo na kushambulia nchi za jirani, suala
lililozipelekea nchi hizo kuunda kikosi cha pamoja kwa ajili ya
kuendesha operesheni kali dhidi ya kundi hilo, operesheni ambazo
zinatajwa kupata mafanikio makubwa hadi sasa.
No comments:
Post a Comment